Tangazo

November 1, 2016

SBL YAZINDUA KAMPENI YA UNYWAJI KISTAARABU MKOA WA ARUSHA


Meneja wa SBL wa Uwajibikaji Katika Jamii, Hawa Ladha akitoa elimu kwa wadau mbalimbali  walioshirki katika mkutano katika uzinduzi wa kampeni ya unywaji kistaarabu  uliofanyika katika Hotel ya Kibopalace mapema wiki iliyopita 

Askari wa barabarani kutoka wilaya za mbali mbali za mkoa wa Arusha ambao pia walihudhuruia mkutano huo  wa uzinduzi wa kampeni ya unywaji wa kistaarabu iliyozinduliwa na SBL na kufanyika katika Hoteli ya KiboPalace katika mkoa wa Arusha mapema wiki iliyopita.

Semina ya unywaji kistaarabu  ikiendelea 

Askari wa usalama  barabarani wakisikiliza kwa makini

Mkuu wa Usalama wa Barabarani wa Mkoa wa Arusha Mhandisi  Nuru Kacharia Seleman akitoa hotuba kwa wadau mbali mbali  waliohudhuria  mkutano wakati wa uzinduzi wa kampeni ya unywaji kistaarabu mkoani Arusha 

Mkuu wa Usalama wa Barabarani wa Mkoa wa Arusha Mhandisi  Nuru Kacharia Seleman akiwa kashika kava la gari akiwa na viongozi wa usalama wa barabarani mkoani arusha na wafanyakazi wa SBL Arusha na wasambazaji wa SBL kuashiria uzinduzi rasmi wa kampeni ya Unywaji kistaarabu iliyozinduliwa na SBL mkoani Arusha katika Hoteli ya Kibo Palace mapema wiki iliyopita

Wadau mbalimbali wakiwa katika  picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa kampeni ya Unywaji wa kistarabu mkoani Arusha.


 Kampuni ya bia ya Serengeti imezindua kampeni inayohamasisha matumizi sahihi ya pombe au unywaji pombe kistaarabu. Kampeni hii ni hatua muhimu katika sekta ya biashara ya pombe kwa kutambua changamoto inazokabiliana nazo hususani katika masuala ya uwajibikaji kwa jamii.  

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Mkuu wa Usalama wa Barabarani wa Mkoa wa Arusha Mhandisi  Nuru Kacharia Seleman, amesema kulishirikisha jeshi la polisi, kikosi cha usalama barabarani, kunaonyesha ni kwa jinsi gani SBL wanatilia maanani suala zima la usalama barabarani hasa matokeo ya ulevi na uendeshaji vyombo vya moto. Uzoefu unaonyesha kwamba watu wengi hujisahau na kujiingiza katika ulevi wa kupindukia  bila kuzingati vyombo vya moto wanavyoendesha.
“Ni jambo lisilopingika kuwa uzembe na unywaji wa pombe kupita kiasi vina athari kubwa kwa jamii. Madhara hayo hayamuathiri mtumiaji wa pombe peke yake, bali uhatarisha maisha na kuathiri mustakabali wa watu wengi” aliongeza Mhandisi Seleman.
“Kwa matinki hiyo, ni janga la jamii nzima – huduma zetu za afya zimeelemewa kwa kiasi kikubwa na wale waliojeruhiwa katika masuala yanayohusiana na ajali na uhalifu; taasisi zetu za masuala ya sheria zimeelemewa vilivyo; uzalishaji unaathirika mno na kwa mlolongo huo, ukuaji wa pato la taifa hubakia kuwa wa kiwango cha chini”, alisema Bi Mhandisi Seleman.
Akielezea jinsi kampeni hii itakavyosaidia Mhandisi Seleman anasema “ama kwa hakika, sote kwa ujumla wetu tunaathirika – na sote tunalo jukumu la kuchangia namna bora ya kukabiliana na tatizo la ulevi. Nafurahi kuona kwamba wazalishaji wenyewe wa vinywaji vya pombe wametambua kuwa biashara wanayofanya kwa wateja wao inahitaji uwajibikaji na umakini wakati wa kutumia”.  
Kampeni hii ya unywaji wa kistaarabu inakusudia kuwafikia vijana wengi pamoja na watu wa rika la juu kwa kuwataka kuelewa hatari ya matumizi ya pombe na kufanya maamuzi kwa faida zao – maamuzi ambayo yatanusuru mustakabali wao wa baadaye.

Naye Meneja wa SBL wa Uwajibikaji Katika Jamii, Hawa Ladha, amesema kampeni ya unywaji pombe kistaarabu inalenga kuwapa walengwa elimu kwamba mtumiaji wa pombe hahitaji kutawaliwa na pombe na kuipa nafasi ibadili mustakabali wa maisha wake na kuongeza kwamba vifo na ajali nyingi hutokana na uzembe au ulevi wa watu ambao si waathirika wakubwa wa pombe – ambao wangeweza kuwa waangalifu kama wangechukua tahadhari na kujifikiria marambili au kama marafiki zao wasingewahamasisha ku-“ongeza moja …au mbili”, alisema.

No comments: