Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiwasili Nansio wilayani Ukerewe kwa meli ya MV. Nyehunge II
ambapo alikuwa na kazi za kuweka jiwe la msinggi kwenye mradi wa maji wa
Nebuye pamoja na kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Chumba cha
Upasuaji kituo cha Afya Kagunguli na kuhutubia wananchi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu
Hassan akiwapungia wananchi wa Nansio wilayani Ukerewe waliojitokeza
kumpokea ambapo aliwasili kutokea Mwanza mjini kwa meli ya MV. Nyehunge
II
ambapo alikuwa na kazi za kuweka jiwe la msinggi kwenye mradi wa maji wa
Nebuye pamoja na kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa Chumba cha
Upasuaji kituo cha Afya Kagunguli na kuhutubia wananchi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akiambatana
na viongozi mbali mbali katika kukagua mradi mkubwa wa maji wa Nebuye
wilayani Ukerewe mkoa wa Mwaza
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akihutubia wakazi wa kijiji cha Nebuye ambapo aliwasihi kuutunza mradi wa maji na mazingira kwa ujumla wakati wa kuweka jiwe la msingi katika mradi wa maji ya Nebuye wilayani Ukerewe mkoa wa Mwaza.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akisoma
maandishi yalioandikwa kwenye jiwe la msingi la mradi mkubwa wa maji wa
Nebuye wilayani Ukerewe mkoa wa Mwaza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akiwapungia wakazi wa kijiji cha Kagunguli wakati akiwasili tayari kuhutubia wakazi wa kijiji hicho.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akihutubia
wakazi wa kijiji cha Kagunguli wilayani Ukerewe na kusisitiza serikali ya awamu ya tano ni ya kufanya kazi kwa bidii ili kuleta maendeleo ya Tanzania.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akihutubia
wakazi wa kijiji cha Kagunguli wilayani Ukerewe.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan akiwasalimia
wakazi wa Nansio waliojitokeza kwa wingi kutaka kumsalimia na kuwakilisha kero
zao wakati wa ziara yake katika wilaya ya Ukerewe
..................................................................
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameweka jiwe la
msingi katika mradi mkubwa wa maji kwenye mji Nansio katika kisiwa cha Ukerewe
mkoani Mwanza mradi ambao utahudumia wananchi elfu 61.
Makamu wa
Rais ambaye amesafiri kwa takribani masaa Matatu na meli ya MV Nyehunge II katika
Ziwa Victoria kwenda kisiwa Ukerewe kwa mara ya kwanza tangu ashike wadhifa
huo,amewahimiza wananchi hao wautunze mradi huo ambao utasaidia kwa kiasi
kikubwa kuondoa tatizo na uhaba wa maji safi na salama katika kisiwa hicho.
Mradi huo ambao
unaojumuisha kazi za uboreshaji wa huduma ya majisafi na usafi wa mazingira unatekelezwa
chini ya umefadhili wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na serikali ya Tanzania katika miji ya Sengerema,Geita na
Nansio – Ukerewe kwa gharama ya Dola za Kimarekani milioni 30.4 ambapo serikali
ya Tanzania imechangia mradi huo Dola za Kimarekani milioni nne.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan amewaahidi wananchi kuwa serikali ya awamu ya Tano unamikakati
mizuri inayolenga kuondoa tatizo la maji kote nchini ili kusaidia wananchi hao hasa wanawake kutumia
muda mwingi kufanya kazi za maendeleo kuliko kutafuta maji.
No comments:
Post a Comment