Tangazo

December 1, 2016

PUMA YANG'ARISHA UTALII ZANZIBAR KWA MASHINDANO YA NDEGE KONGWE 22

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Phillipe Corsaletti (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Rubani wa kike mdogo kuliko marubani wote wa ndege ya zamani, Sara Meehan (18), jinsi injini ya ndege hiyo kutoka Botswana inavyofanya kazi, wakati wa mapokezi  ya ndege hizo 'Vintage Air Rally' kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume, Zanznibar jana. Ndege hizo zilitengezwa kati ya mwaka 1920 na 1930. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Phillipe Corsaletti (kushoto), akisalimiana na rubani wa ndege ya zamani Pedro Langton kutoka Canada, wakati wa mapokezi ya mashindano ya ndege 22 za zamani 'Vintage Air Rally' kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume, Zanznibar jana. Kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Dk. Miray Ussi
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Phillipe Corsaletti (kushoto), na Mkurugenzi wa Masoko wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Dk. Miray Ussi wakiangalia ndege ya zamani kutoka Canada, wakati wa mapokezi ya mashindano ya ndege 22 za zamani 'Vintage Air Rally' kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume, Zanznibar jana.
 Rubani akishuka kutoka kwenye ndege
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Phillipe Corsaletti (kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya Puma, Ben Moshi wakiangalia moja ya ndege hizo za zamani, wakati wa mapokezi ya mashindano ya ndege 22 za zamani 'Vintage Air Rally' kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume, Zanznibar
 Ndege ya zamani ya Afrika Kusini ikiwasili Zanzibar
 Ndege ya zamani ya Uingereza ikiwasili uwanajani Zanzibar
 Ndege ya zamani ya Canada ikiwasili Zanzibar
 Baadhi ya ndege kongwe zikiwa zimejipanga Uwanja wa Ndege wa Abeid Aman Karume

 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Phillipe Corsaletti (kushoto), na Mkurugenzi wa Masoko wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Dk. Miray Ussi wakiangalia ndege ya zamani
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Phillipe Corsaletti (kushoto), akizungmza na mmoja wa marubani wa ndege hizo
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Phillipe Corsaletti (kushoto), akihutubia wakati wa mapokezi ya ndege hizo.
 Mkurugenzi wa Masoko wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar, Dk. Miray Ussi, akitoa shukrani kupangwa kwa ndege hizo kutua Zanzibar
 Mkurugenzi wa mashindano na ndege hizo Vintage Air Rally, Sam Rutherford akielezea kuhusu mashindano hayo pamoja na kutoa shukrani kwa Kampuni ya Puma kuwafadhili kwa kutoa mafuta kwenye ndege hizo
 Wakati wa mkutano huo
  Meneja Rasilimali Watu wa Puma Tanzania Bi Loveness Hoyange (kulia) akiwa na Rubani wa kike mdogo kuliko wote katika mashindano hayo, Sara
  Meneja Rasilimali Watu wa Puma Tanzania Bi Loveness Hoyange (kulia0 akiwa na mfanyakazi mwenzie wakati wa mapokezi ya ndege hizo.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Phillipe Corsaletti na Wafanyakazo wa kampuni hiyo wakiwa katika puicha ya pamoja na marubani wa ndege hizo.
 Watalii wakiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Abeid Aman Karume, Zanzibar

 Ndege ya zamani ya Uingereza ikiwasili uwanjani
Moja ya ndege kubwa ya zamani ikiwasili kwenuy e Uwanja huo

Zanzibar, 30 Novemba 2016 – Mashindano ya “Vintage Air Rally’ yamewasili  salama Tanzania tarehe 28/11/2016 wakitokea uwanja wa Ndege wa Wilson, Nairobi kama ilivyokuwa imepangwa, na wafanyakazi wa Puma Energy Tanzania kitengo cha mafuta ya ndege walizihudumia ndege hizi kwa kuzijaza mafuta aina ya Avigas katika uwanja wa Ndge wa Arusha. 

Baada ya hapo ndege hizo ziliruka hadi mbuga ya wanyama ya Ngorongoro ambapo ilikuwa sehemu ya safari yao. Leo wanaporuka kuja Zanzibar, Kampuni ya Puma Energy Tanzania inajisikia fahari kuyakaribisha haya mashindano katika visiwa vizuri vya marashi ya Zanzibar, ambapo waalikwa mbalimbali kutoka Serikalini, Balozi mbalimbali, Puma Energy yenyewe, na wageni mbalimbali watakua na fursa ya kukutana na marubani wanaoshiriki shindano hili pamoja na ndege zenyewe, na baadaye kuwa na tafrija ya pamoja katika Hoteli ya Hyatt iliyoko mji Mkongwe.

Kampuni ya Puma Energy inayofuraha kuwa mwenyeji wa mashindano haya.   Tumejikita katika kuendelea kufanya vyema na pia kuwa na uhakika wa upatikanaji wa bidhaa ya mafuta na tunafuraha kutoa mchango wetu katika kuhakikisha kwamba mashindano yanafanyika vyema. Jukumu letu katika kusaidia kuendeleza utalii ndani ya nchi yetu linabaki kuwa sehemu muhimu sana katika masuala yetu ya kijamii kama kampuni katika kutimiza majukumu yetu ya kila siku”, Alisema Philippe Corsaletti, Meneja Mkuu wa Puma Energy Tanzania.

Vintage Air Rally inahusisha ndege za zamani za kati ya miaka ya 1920 na 1930 ambazo zinarushwa na marubani wenye uzoefu mkubwa kutoka sehemu mbalimbali duniani, wakiruka kukatisha Afrika kutoka katika visiwa vya Crete nchini Ugiriki hadi Cape Town Afrika ya Kusini. 

Shindano hili lilianza tarehe 12/11/2016 kule Crete, Ugiriki na safari yote itachukua siku 35  wakipita katika jumla ya nchi 10 ambazo ni Ugiriki, Misri, Sudan, Ethiopia, Kenya, Tanzania na kuendelea Zambia, Zimbabwe, Botswana na Afrika ya Kusini.

Kampuni ya Puma Energy Tanzania imejiandaa vizuri kupokea ugeni huu ikiwa ni pamoja na kuhakikisha huduma zote za kujaza mafuta ili kuhakikisha urukaji ulio salama. Ndege hizi zinatumia mafuta aina ya Avgas tu na kampuni ya Puma ambayo pekee inayotunza mafuta hayo hapa Nchini, itazihudumia ndege hizi wakati wote zitakapokuwa nchini. 

“Timu ya watu wetu imejiandaa kupokea na kuhudumia msafara mzima katika kiwango cha juu cha ubora na ufanisi. Uwepo wa bohari zetu za mafuta ya ndege katika maeneo mbalimbali nchini unafanya iwe rahisi kuhudumia ndege hizo ambao msafara huu utapita,” Alisema Corsaletti. 

Kwa hapa Tanzania, Vintage Air Rally Aircrafts zitatua ili kujaza mafuta Kilimanjaro, Arusha, Dar es salaam, Zanzibar, Dodoma, and Songwe kabla ya kuelekea Zambia ambapo watapokelewa na kuhudumiwa na wenzetu wa Puma Zambia. 

Tanzania itaweka historia kwa kuwa moja ya nchi chache duniani ambapo mashindano haya yatapita. “Tunawakaribisha wananchi wote katika tukio hili la kihistoria wakati ndege za Vintage zitakapokua zikipita maeneo yao kwa kuwa tukio hili litasaidia kukuza utalii”. 


Kuhusu njia itakayotumika:

Njia inayotumika ni sawa kabisa na ufuatishaji wa safari ya shirika la ndge la Imperial ya mwaka 1931 “safari ya Afrika” ambapo ndege itakua ikiruka chini kupitia Nile kutokea Kairo hadi Khartoum, kupitia milima ya Ethiopia, uwanda wa chini wa Kenya,  na hatimaye sehemu yenye changamko sana ya Afrika Mashariki.

  Baada ya hapo itaondoka tena kupitia Kilimanjaro hadi Serengeti, na hatimaye hadi kwenye visiwa vya marashi ya Zanzibar na hadi chini Zaidi, kupitia Zambia, juu ya maporomoko ya Victoria, hadi Bulawayo Zimbabwe. 

Siku za mwisho za safari hii ndefu inayohitaji pumzi nyingi itawafikisha Botswana na Afrika ya Kusini - Capetown ambapo utakua mwisho wa safari. 

Kampuni ya Puma Energy ni kampuni ya kimataifa ya viwango vya kati ambayo imejikita katika kusafisha mafuta ghafi, kutunza na kusambaza mafuta masafi kwa watumiaji katika zaidi ya nchi 45 duniani. 

Puma ilingia Tanzania mwaka 2012 na hadi sasa inaongoza katika  soko na pia kampuni pekee yenye uwepo katika viwanja vinane hapa Tanzania  ambavyo ni Kilimanjaro, Zanzibar, Songwe, Mwanza, Tabora, Dodoma, Arusha, na Julius Nyerere. 


Philippe Corsaletti

Meneja Mkuu

No comments: