Tangazo

January 25, 2017

MFANYABIASHARA WA MADINI KORTINI KWA KUMPIGA CHUPA MKEWE MBELE YA BABA MKWE

Na Woinde Shizza,Arusha


Mfanya biashara maarufu wa madini  jijini Arusha, Venance  Moshi (30)amefikishwa Mahakamani na kusomewa maelezo ya awali katika kesi  inayomkabili ya kushambulia na kumjeruhi  mkewe kwa chupa usoni, wakiwa wanasuluhishwa na baba mkwe, mgogoro wa ndoa yao.

Mbele ya hakimu , Devota Msofe wa mahakama ya wilaya Arusha, mwendesha
mashtaka wa serikali ,Agnesi Hyera alieleza mahakama hiyo kuwa mnamo machi 11 mwaka 2016 katika maeneo ya Moshono kwenye usuluhishi wa mgogoro wa ndoa yao ,mshtakiwa alinyanyua glasi na kumpiga kwenye jicho la kulia mlalamikaji (mkewe) Agnesi Joseph (30)iliomjeruhi vibaya.

Mwendesha mashitaka aliieleza mahakama hiyo kuwa kuwa hatua hiyo ilimsabishia mlalamikaji atokwe na damu nyingi na baadae kutoa taarifa


kituo cha polisi ambapo mtuhumiwa alitiwa mbaroni na baadae kufikishwa
mahakamani.

Baada ya kusomewe maelezo hayo mshitakiwa  huyo alikana mashtaka ,na hakimu Msofe  alipanga siku ya kuanza kusikilizwa kwa shauri hilo,baada ya upande wa Jamhuri kudai kuwa wapotayari kwa usikilizwaji wa kesi hiyo.

Katika shauri hilo la jinai namba 438 la mwaka 2016 ,upande wa jamhuri
unatarajia  kuwasilisha mashahidi watatu na vielelezo kadhaa ikiwemo hati
ya polisi(PF3), hati ya daktari pamoja na picha za jeraha. Kesi hiyo
imepangwa kusikilizwa february  6, mwaka huu, saa tatu asubuhi.

Aidha katika hatua nyingine ,shahidi namba moja wa kesi hiyo ,Agnes Joseph
anatarajia kufungua kesi nyingine ya kudai talaka kwa mumewe huyowaliyefunga naye ndoa mwaka 2012 baada ya ndoa yao kukumbwa na migogoro ya mara kwa mara huku akiambulia kipigo na vitisho.

 
Alisema  ameishi na mumewe huyo katika mazingira ya migogoro na wamekuwa wakisuluhishwa mara kadhaa bila mafanikio.

No comments: