Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Francis
Massawe akizungumza baada ya kuzindua
duka la Airtel Mkoani Manyara hivi karibuni, Anayeshuhudia Meneja wa
Airtel mkoa wa Manyara Peter Kimaro.
|
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
- Jumla ya maduka matatu
kuzindualia katika maeneo ya Babati mjini Dareda center na Riloda mkoani
humo
Kampuni ya simu za mikononi ya Airtel imezindua duka mjini
Babati kwa ajili ya kutoa huduma kwa wateja wanaoishi katika maeneo mbali mbali
ya mkoa wa Manyara ikiwa ni mwendelezo wa mpango wake wa kufungua maduka ya
kutoa huduma kwa wateja wake nchi nzima.
Kamanda wa polisi mkoa wa
Manyara,Fransic Masawe,ndiye aliyezindua duka hilo ambaye amesema litasadiai
kutoa huduma kwa wakati lakini pia lisaidia kutoa ajira kwa vijana na kuwawezesha wakulima wa
mazao ya kupata huduma za kifedha kwa
urahisi zaidi
“Nawapongeza Airtel kwa kusogeza huduma karibu
na wateja na kuongeza kuwa duka hilo
litakuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa mji wa Babati pamoja
na maeneo jirani. Napenda kuchukua fursa hii kuwa kuwaasa wakazi wa hapa
hususani vijana kuchangamkia fursa za ajira zilizopo kupitia duka hilo ajira
kwa lengo lakujiongezea kipato”, Alisema Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara,
Fransic Masawe.
Kwa Upande wake Meneja wa Airtel mkoa wa
Manyara,Peter Kimaro,amesema duka hilo linalenga kusogeza huduma karibu na
jamii kwani kipindi cha nyuma wananchi walikuwa wanapata tabu kupata huduma za
uhakika lakini pia hatua hiyo inatoa mwanya wakuongeza maduka mengine mengi
katika maeneo ya mkoa huo ikiwemo wilaya ya Katesh
Pia amesema huduma ya mawasiliano ni chachu ya maendeleo
kwani inasaidia uendeshaji wa shughuli za kiuchumi na kuwawezesha huduma za
kifedha kupatikana kirahisi ambapo kwa sasa watu wengi hutumia Airtel Money
kufanya miamala pamoja na kupata mikopo kupitia huduma ya Airtel Timiza ambayo
imekuwa ni mkombozi kwa wajasiriamali wadogo wadogo kupata mitaji ya kuendesha
biashara zao.
Tunatoa wito kwa wateja wetu kutembelea maduka haya ambayo
tunayafungua nchi nzima ili kupata huduma hapa manyara tayari tunayo maduka
matatu ambayo moja tunalizindua hapa na mengine mawili yapo katika maeno ya Dareda center na Riloda .aliongeza Kimaro.
Baadhi ya wananchi wamesema kufunguliwa kwa duka hilo
kutaongeza ajira kwa vijana pamoja na kutoa huduma za uhakika za miamala ya
fedha na mawasiliano kwa ujumla tofauti na kipindi cha nyuma ambapo walikuwa
wanalazimika kufuata huduma umbali mrefu kidogo.
Kampuni ya
Airtel inampango wakuongeza maduka mengine katika mkoa huo wa Manyara ili
kuendelea kusogeza huduma zake kwa wateja kwa urahisi hususani katika maeneo ya
vijijini.
No comments:
Post a Comment