Tangazo

May 25, 2017

MAADHIMISHO YA SIKU YA AFRIKA, WAUZAJI WA BIDHAA ASILI JIJINI MWANZA WANENA

Mei 25 kila mwaka Mataifa mbalimbali Barani Afrika huadhimisha Siku ya Afrika kama sehemu ya mataifa hayo kukumbuka ukombozi wake barani Afrika.

Jijini Mwanza, watengenezaji na wauzaji wa vitu vya kitamaduni wamewataka watanzania kuongeza kasi ya matumizi ya vitu hivyo badala ya kutegemea vitu kutoka mataifa ya Maghabiri.
#BMGHabari
Kulia ni Mzee Francis Gabriel pamoja na Bi.Salome Babae ambao ni watengenezaji na wauzaji wa bidhaa za asili wakiwa kwenye eneo lao la biashara. Wanapatikana eneo la darajani Jijini Mwanza. Mawasiliano yao ni 0783 83 83 73
George Binagi-GB Pazzo
Watanzania wameshauriwa kupenda kutumia bidhaa za asili ikiwemo mavazi na urembo ili kuondoakana na utumwa wa kutovipa thamani vitu hivyo.

Wauzaji wa vitu vya asili katika eneo la darajani jijini mwanza, wayasema hayo wakati wakizungumza na lake fm kuhusiana na maadhimisho ya siku ya afrika hii leo.

Maadhimisho ya siku ya afrika yalianza kuadhimishwa tangu mei 25 mwaka 1963 yakilenga kuyahamasisha mataifa ya bara la afrika kujikomboa kutoka utumwani hususani kiakiri na kifira ili kuthamini zaidi tamaduni za kiafrika.

No comments: