Naibu Waziri wa Kazi,Ajira na Watu wenye Ulemavu, Anthony Mavunde, (wa pili kulia) akikabidhi Kombe la SportPesa Super Cup kwa Nahodha wa Gor Mahia, Shakava Haron, baada ya timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya AFC Leopards katika mchezo wa fainali uliochezwa Juni 11 kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.
Na Ripota wa Mafoto Blog, Dar
Timu ya Gor Mahia ya Kenya imetwaa ubingwa wa kwanza wa
mashindano ya SportPesa Super Cup baada ya kuwasambaratisha wapinzani wao, AFC
Leopards kwa mabao 3-0 kwenye uwanja wa Uhuru. Uliozikutanisha timu zote za Kenya uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji wa Gor Mahia na mfungaji wa bao la kwanza kati ya matatu, Muguna Kenneth, akimtoka beki wa AFC Leopards, Abdallah Salim, wakati wa mchezo wa Fainali wa mashindano ya SportPes Super Cup.
*********************************************
Kwa ushindi huo, Gor Mahia ilizawadiwa Sh milioni 62 za
Tanzania huku AFC Leopards ikiambulia Shilingi Milioni 22 kwa kushika nafasi ya
pili.
Mabao ya Timotho Otieno katika dakika ya 60, OliverMaloba
katika dakika ya 76 na John Ndirangu katika muda wa nyongeza yalitosha
kuinyamazisha AFC Leopards kwenye fainali hiyo iliyokuwa ya kusisimua.
Mshambuliaji wa Gor Mahia, Muguna Kenneth (kushoto) akimtoka beki wa AFC Leopards, Ramadhan Yakubu, wakati wa mchezo wa Fainali wa mashindano ya SportPes Super Cup, uliozikutanisha timu zote za Kenya uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
****************************************************
Dalili za ushindi kwa Gor Mahia zilionekana tokea mwanzoni mwa mchezo huo ambapo mshambuliaji wake hatari, Medie Kagere alikosa baola wazi baada ya pasi nzuri ya GeorgeOdhiambo.
Wachezaji wa Gor Mahia wakishangilia bao la pili
Mshambuliaji wa Gor Mahia, Muguna Kenneth (kulia) akimtoka beki wa AFC Leopards, Abdallah Salim, wakati wa mchezo wa Fainali wa mashindano ya SportPes Super Cup, uliozikutanisha timu zote za Kenya uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji wa Gor Mahia, Kagere Medie, akiruka kupiga mpira wa kichwa langoni kwa AFC Leopards, wakati wa mchezo wa Fainali wa mashindano ya SportPes Super Cup, uliozikutanisha timu zote za Kenya uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Beki wa AFC Leopards, Abwao Marcus (kushoto) akiwania mpira na mshambuliaji wa Gor Mahia, Wafula Innocent, wakati wa mchezo wa Fainali wa mashindano ya SportPes Super Cup, uliozikutanisha timu zote za Kenya uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Beki wa AFC Leopards, Ramadhan Yakubu, akiruka katikati ya wachezaji wa Gor Mahia kuokoa mpira, wakati wa mchezo wa Fainali wa mashindano ya SportPes Super Cup, uliozikutanisha timu zote za Kenya uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Kipa wa Gor Mahia, Odhiambo Fredrick (kushoto) akipokea zawadi ya kipa bora wa mashidnao
Kagere Medie (kushoto) akipokea zawadi ya mfungaji bora wa mashindano
Wachezaji wa AFC Leopards, wakivishwa medali
Viongozi wa AFC Leopards wakipokea mfano wa hundi ya Dola 10,000/=
Wachezaji wa Gor Mahia wakivishwa medali na Waziri Mavunde
Viongozi wa Gr Mahia wakipokea mfano wa hundi ya Dola 30,000/=
Gor Mahia wakiwa katika picha ya pamoja na kombe lao.
No comments:
Post a Comment