Tangazo

June 29, 2017

Serikali, Wadau wa Habari wakubaliana kujenga uhusiano imara kikazi

Wadau wa Habari nchini wakiongozwa na Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania kwa kushirikiana na Wakfu wa Taasisi Huru za Uwazi Afrika (OSIEA) wamefanya semina ya siku moja kwa lengo la kuboresha mahusiano ya utendaji wa kazi iliyoshirikisha Serikali na wadau wa habari nchini.

Semina hiyo pia ilihudhuriwa na maafisa wa Serikali wakiongozwa na Naibu Waiziri wa Habari, Utamaduni, Michezo na Wasanii Bi Annastazia Wambura, Wabunge, wawakilishi wa vyuo vikuu, viongozi wa taasisi za Habari nchini, wahariri na waandishi.

Naibu Waziri, Anastazia Wambura akizungumza kwenye mkutano huo amesema serikali iko bega kwa bega na waandishi wa habari ili kufikia malengo waliyojiwekea katika kuhabarisha umma.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura akizungumza kwenye mkutano wa wadau mbalimbali wa habari waliokutana kujadili namna ya kufanya kazi kwa pamoja na Serikali ili kuleta ustawi wananchi leo kwenye ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Usajili wa Magazeti, Bw. Patrick Kipangula akiwasilisha mada kuhusu sheria ya vyombo vya habari aliyoiwasilisha kwenye mkutano wa wadau wa vyombo vya habari waliokutana na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura.
Mjumbe wa Bodi ya MISA Tanzania, James Marenga akizungumza kuhusu umuhimu wa vyombo vya habari hasa kwenye sheria ya vyombo vya habari.
Mhariri Mtendaji wa The Guardian Ltd, Jesse Kwayu akiwasilisha mada kuhusu namna ya kufanya mahusiano ya kikazi kati ya serikali na wanahabari kwa baadhi ya wabunge, wahariri, Maafisa habari na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Zamaradi Kawawa(kushoto) akitolea ufafanuzi baadhi ya mambo  yanayohusu Idara ya Habari Maelezo yaliyoulizwa na wadau wa habari kwenye mkutano uliowakutanisha wadau mbalimbali wa habari waliokutana leo kwenye ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma. Katikati ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Anastazia Wambura.
Mhadhiri Msaidizi kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam, Paul Dotto Kuhenga akiwasilisha mada kwa wahariri, waandishi wa habari na maafisa habari wa Serikali waliokutana kujadili njia bora ya kufanya kazi kwa pamoja leo kwenye ukumbi wa Hazina Ndogo mjini Dodoma.
Afisa Habari na Utafiti wa MISA-Tanzania, Sengiyumva Gasirigwa akizungumza jambo mbele ya baadhi ya wabunge na baadhi ya wahariri, waandishi wa habari pamoja na wadau mbalimbali wa vyombo vya habari waliofika katika semina ili kujadili jinsi ya kutengeneza mahusiano ya kikazi kati ya Serikali na wanahabari yatakayoleta ukaribu kwa pande zote. 
Baadhi ya wadau mbalimbali wa vyombo vya habari wakichangia mada kuhusu namna ya kushirikiana kati ya Serikali na vyombo vya habari hapa nchini ili kuleta ufanisi katika tasnia ya habari.
Baadhi ya wadau mbalimbali wa vyombo vya habari wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinawasilishwa kushirikiana kati ya Serikali na vyombo vya habari hapa nchini ili kuleta ufanisi katika tasnia ya habari.
Picha ya pamoja

No comments: