Tangazo

July 13, 2017

Jamii Media na CIPESA wakutanisha Wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano

Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence Mello (wa pili kulia) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumalizika kwa kongamano la wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) nchini Tanzania, lililoandaliwa na Kampuni ya Jamii Media ya Tanzania wamiliki wa mitandao ya Jamii Forums na Fikra Pevu kwa kushirikiana na Kampuni ya CIPESA ya nchini Uganda. Wengine ni Mkurugenzi wa CIPESA, Dk. Wairagala Wakabi ( kulia) na Mkurugenzi wa Jamii Media, Mbaraka Islam (kushoto). Kongamano hilo lilifanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence Mello (wa pili kulia) akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kumalizika kwa kongamano la wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) nchini Tanzania, lililoandaliwa na Kampuni ya Jamii Media ya Tanzania wamiliki wa mitandao ya Jamii Forums na Fikra Pevu kwa kushirikiana na Kampuni ya CIPESA ya nchini Uganda. Wengine ni Mkurugenzi wa CIPESA, Dk. Wairagala Wakabi (wa kwanza kulia) na Mkurugenzi wa Jamii Media, Mbaraka Islam (kushoto). Kongamano hilo lilifanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Mmoja wa washiriki katika kongamano hilo, Joseph Ngwegwe-mdau wa ICT akijadili jambo katika mjadala wa wadau wa ICT, wengine ni Robert Madziva- Maxcom Africa (kulia) na Chambi Chachage wakiwa katika mjadala huo. Mmoja wa washiriki katika kongamano hilo, Catherinerose Barretto (wa kwanza kulia) akizungumza katika mjadala na wadau wa ICT kwenye kongamano hilo. Kutoka kushoto ni Chambi Chachage-Udadisi Blog, Joseph Ngwegwe-mdau wa ICT pamoja na Robert Madziva- Maxcom Africa wakiwa katika mjadala huo. Meneja Mkuu wa Kampuni ya Jamii Media, Asha Abinallah akizungumza na washiriki wa kongamano la wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) nchini Tanzania.

  KAMPUNI ya Jamii Media ya Tanzania wamiliki wa mitandao ya Jamii Forums na Fikra Pevu kwa kushirikiana na Kampuni ya CIPESA ya nchini Uganda imefanya kongamano la kuwakutanisha wadau wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) nchini Tanzania ikiwa ni kujadili masuala mbalimbali ya huduma za habari na mawasiliano pamoja na kuangalia namna ya kulinda usiri wa taarifa za wateja wanaotumia huduma hizo.

 Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa kongamano hilo, Mkurugenzi Mtendaji wa Jamii Media, Maxence Mello alisema kongamano hilo limekuwa na matokeo chana baada ya wadau kujadili masuala mbalimbali ya ICT lengo likiwa kuboresha zaidi huduma hiyo na usalama kwa watumiaji.

 Alisema wadau wengi kwenye kongamano hilo wameunga mkono hatua ya uwekaji wa sheria za kusimamia huduma nzima ya ICT lakini wakashauri ufanywe kwa kutoa fursa za maendeleo na si kuminya ubunifu wala uhuru na usiri wa watumiaji wa huduma za ICT.

 Alisema wadau wengi katika kongamano hilo walihoji kitendo cha Sheria ya Makosa ya Mtandao (The Cyber Crimes Act, 2015) kuanza kutumika bila ya uwepo wa kanuni jambo ambalo limewapa ugumu hata watekelezaji na wasimamizi wa sheria husika. 

Mkurugenzi huyo aliongeza Jamii Media itaendelea kusaidia kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali wa huduma za mawasiliano wakiwemo bloggers ili kuona wanakuwa na uelewa na matumizi mazuri ya mitandao yao kupunguza mkanganyiko kwa wanufaika.   Maria Sarungi (kushoto) Mkurugenzi Uzalishaji kutoka 'Compass Communications Ltd' akiongoza majadiliano kwenye kongamano hilo. Mmoja wa washiriki katika kongamano hilo, Catherinerose Barretto (wa kwanza kulia) akizungumza katika mjadala na wadau wa ICT kwenye kongamano hilo. Kushoto ni Robert Madziva- Maxcom Africa wakifuatilia mjadala huo.

No comments: