NA
K-VIS BLOG/Khalfan Said
MAMIA
ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na viunga vyake (pichani juu), wamefurika
kwenye banda la PSPF kwenye maonesho ya 41 ya biashara ya Kimataifa ya Dar es
Salaam yanayoandaliwa na Mamlaka ya Undelezaji biashara nchini (Tan Trade)
kwenye viwanja vya Julius Nyerere barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Wengi
wa wananchi hao ni pamoja na wastaafu, wafanyakazi wa umma na binafsi ambao
walifika kupata huduma mbalimbali lakini kubwa iliyovutia wengi kuuliza maswali
ni jinsi ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS) unaomuwezsha mtu
yoyote aliye kwenye sekta rasmi na isiyo rasmi ili mradi awe na kazi
inayomuinguizia kipato.
Akijibu
maswali ya waliohitaji kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari, Meenja wa
Mpango huo, Bi. Mwanjaa Sembe alisema, kujiunga na mpango hyuo ni bure na mtu
atakayejiunga atahitajika kuchangia shilingi kiwango chochote kila mwezi ambapo
kiwango cha chini kabisa ni shilingi elfu kumi (10,000) tu.
Alisema
mpango wa uchangiaji wa hiari licha ya kumuwezesha mwanachama kujiwekea akiba
yake, lakini pia anafaidika na mafao mbalimbali ikiwemo fao la bima ya afya. Fao
la elimu, fao la ujasiriamali, fao la uzeeni, fao la kujitoa na mikopo ya
nyumba na viwanja, haya yote yatategemea na jinsi unavyojiwekea akiba
(michango)
Waziri
wa Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage, (kushoto), akipokea zawadi ambayo
ni taarifa mbalimbali za Mfuko wa Pensheni wa PSPF, kutoka kwa Meneja wa Mpango
wa uchangiaji wa Hiari, 9PSS), Bi. Mwanjaa Sembe, wakati alipotembelea banda la
Mfuko huo Julai 1, 2017. Kulia ni Afisa Uhusiano wa Mfuko huo, Bi Coletha
Mnyamani. Wakwanza kushoto ni Mkuu wa Mawasiliano ya Serikali wizara ya Fedha na Mipango, Bw. Ben Mwaipaja.
Afisa Uhusiano wa Mfuko huo, Bi Coletha
Mnyamani, (kushoto), akimuhudumia mwananchi.
Afisa
wa Polisi aliyefika kujua michango yake akipatiwa huduma na Afisa uendeshaji wa PSPF, Bw.Miteko Chaula.
No comments:
Post a Comment