Tangazo

July 19, 2017

MAOFISA UGANI WA WILAYA YA BUKOMBE WATAKIWA KUWA NA KUMBUKUMBU ZA KILIMO


 Mkuu wa wilaya ya Bukombe,. Joseph Maganga (kulia), akizungumza na maofisa Ugani wa Wilaya hiyo kwenye mafunzo ya kilimo cha mazao ya Mihogo,Pambana Viazi lishe yaliyoandaliwa na Tume yaTaifa yaSayansi na Teknolojia(COSTECH) kupitia Jukwaa la Bioteknolojia OFAB. Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wa wilaya hiyo, Zacharia Bwile na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Baraka Maganga.

Mshauri wa Jukwaa la Masuala ya Bioteknolojia (OFAB) Dk. Nicholaus Nyange, akitoa mada kuhusu matumizi ya Bioteknolojia ya kilimo.

Maofisa Ugani wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Ofisa Kilimo na Umwagiliaji wa wilaya hiyo, Joseph Machibya akizungumza katika mafunzo hayo.
Mratibu wa Jukwaa la Bioteknolojia Tanzania (OFAB), Philbert Nyinondi (kulia), akifuatilia mafunzo hayo. Kutoka kushoto ni Waandishi wa habari zakilimo, Gelard Kitabu na Carvin Gwabara.
Mtafiti wa kilimo kutoka COSTEC, Bestina Daniel akizungumza kwa niaba wa Mkurigenzi Mkuu wa Costech wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo.
Maofisa Ugani wa Wilaya ya Bukombe wakiwa kwenye mafunzo hayo.
Wanahabari wakiwa kwenye mafunzo hayo.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Baraka Maganga akizungumza kwenye mafunzo hayo. 
Mtafiti wa Kilimo kutoka Kituo cha Ukiriguru Mwanza, Bakar Chirimi akitoa mada kwenye mafunzo hayo.
Watafiti wa kilimo na maofisa Ugani wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Joseph Maganga.

Na Dotto Mwaibale, Bukombe

MAOFISA Ugani wa Kata na vijiji katika Wilaya ya Bukombe Mkoa wa Geita wametakiwa kuwa na kumbukumbu sahihi za kilimo ili iwe rahisi kufanya kazi yao kwa ufanisi.

Mwito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Bukombe,Joseph Maganga wakati akifungua  mafunzo ya kuwajengea uwezo maofisa hao kwenye kilimo cha mazao ya Mihogo,Pamba na 
Viazi lishe yaliyoandaliwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), kupitia Jukwaa la Bioteknolojia (OFAB).

"Ni vizuri kila ofisa ugani akawa na kumbukubu sahihi za wakulima,mazao,mifugo na  uzalishaji wa mazao kwenye maeneo yake ili kuwezesha kutumia takwimu hiyo kwenye 
shughul mbalimbali za kuboresha sekta ya kilimo" alisema Maganga.


Maganga alisema maofisa ugani wengi hawana kumbukumbu zinazohusu kilimo na ufugaji  kwenye maeneo yao hivyo inapotokea taarifa hizo zikahitajika kwenye kuandaa 
mipango mbalimbali ya kuwezesha sekta hiyo kwenye maeneo yao ndipo huanza  kuhangaika kuzitafuta na wengine hubuni hali ambayo inachelewesha na kuharibu  mipango ya wilaya na wadau wa kilimo.

Amewataka maofisa ugani hao kila mmoja kuwa na taarifa zote za kilimo na idadi ya  wakulima na wafugaji na aina ya shughuli ya kilimo wanayoifanya ili iwe rahisi  kufanya kazi zao.

Maganga ameishukuru Costech kupeleka mafunzo hayo kwenye wilaya yake kwani  anaamini yatasaidia sana kuwarudisha maofisa hao kwenye mstari kama ambavyo  walivyokuwa wakati wanatoka vyuoni maana wanapofika kwenye maeneo ya kazi huanza 
kufanya kazi kwa mazoea kutokana na kubadirishwa na mazingira wanayoyakuta.


Amewataka wataalamu hao wa kilimo kutatua changamoto zingine za kilimo kwenye kata  zao ikiwemo zile za kimasoko hususani madalali ambao wanawanyonya wakulima kwa 
kununua mazao yao kwa bei ndogo na wao kuyauza kwa bei kubwa hali ambayo inashusha ya wakulima kuendelea kuzalisha.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo,  Baraka Maganga amewataka wataalamu hao wa kilimo  kwenda kuitumia elimu waliyoipa kuleta mabadiliko kwenye kilimo kwa wakulima wa 
wilaya hiyo kwa kuwapa mbinu bora za kilimo ili kuongeza tija.

Alisema Halamshauri hiyo itaendelea kushirikiana na kufuatilia kwa makini  utekelezaji wa kazi zao hususani mbinu hizo wanazopewa ili zisiishie kwenye  makabrasha badala yake zifike kwenye maeneo yao ya utawala kama walivyopewa.

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Costech,Bestina Daniel alisema mafunzo hayo ni  moja ya utekelezajiwa kazi za COSTECH za kuwawezesha wakulima na wagani katika 
kutumia mbinu na teknolojia bora za kilimo kwenye uzalishaji ili kuongeza tija na  kupunguza umasikini kwenye kaya.


Alisema Costech ndio wenye dhamani ya kuishauri Serikali kwenye masuala yote  yanayohusu Sayansi na Teknolojia hivyo pale kunapotokea teknolojia na mbinu nzuri  ambazo zinaweza kuleta mageuzi kwenye uzalishaji kwa wakulima hutafuta mbinu 
mbalimbali za kuzifikisha kwa wahusiaka.

Aliongeza kuwa  ili kufikia kwenye uchumi wa viwanda lazima malighafi za kutosha  ziwepo ili kulisha viwanda hivyo na kuzalisha bidhaa hivyo mazao hayo ambayo  Costech inayahamasisha yatasaidia sana katika kulisha viwanda vya nguo,usindikaji wa mihogo na viazi lishe ambavyo vina umuhimu mkubwa kwenye kuongeza lishe na  usalama wa chakula.

Mafunzo hayo ya siku moja kwa maofisa ugani hao yanalenga kuwapatia mbinu bora za  uzalishaji wa mazao ya Mihogo,Viazi lishe pamoja na Pamba na nafasi ya matumizi  bioteknolojia kwenye kuongeza uzalishaji na kutatua changamoto za kilimo kama  magonjwa,wadudu na matatizo ya mabadiliko ya tabia nchi.



No comments: