Tangazo

August 31, 2017

TMA yawajengea uwezo wanahabari kuhusu uandishi wa habari za hali ya hewa

 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk Agnes Kijazi (kulia) akizungumza alipokuwa akifungua semina ya kwa baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari juu ya uandishi wa habari za hali ya hewa. Wengine kutoka kulia ni Bi. Mariam Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Huduma Saidizi wa TMA na Mkurugenzi Huduma za Utabiri TMA, Dk. Hamza Kabelwa. 

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk Agnes Kijazi (kulia) akizungumza alipokuwa akifungua semina ya kwa baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari juu ya uandishi wa habari za hali ya hewa. Wengine kutoka kulia ni Mkurugenzi Matumizi Matumizi ya Hali ya Hewa, Dk. Ladslaus Chang'a , Meneja Ofisi Kuu ya Utabiri, Samwel Mbuya, pamoja na Mkurugenzi Huduma za Utabiri TMA, Dk. Hamza Kabelwa.

  MAMLAKA ya Hali ya Hewa nchini Tanzania leo imewapa semina baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari juu ya uandishi wa habari za hali ya hewa. 

Akizungumza wakati akifungua semina hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Dk Agnes Kijazi alisema semina hiyo ni utaratibu wa TMA kuwajengea uwezo wanahabari ili waweze kuwa mabalozi wa zuri wa kutoa elimu kwa umma juu ya matumizi mazuri ya taarifa za utabiri wa hali ya hewa zinazotolewa na TMA kwa wananchi. 

 Alisema wanahabari inabidi wazielewe vizuri, kuzichambua na kuwafikishia taarifa za utabiri wa hali ya hewa kiusahihi wananchi jambo ambalo litasaidia wananchi na sekta mbalimbali kujipanga kukabiliana na ama athari zitokanazo na utabiri wa hali ya hewa. "...Semina kama hizi kwanza zinasaidia wanahabari kuelewa masuala mbalimbali yatokanayo na taarifa zetu za utabiri, kisha wao kuelimisha jamii zaidi kuhusiana na taarifa zetu kupitia vyombo vyao mbalimbali vya habari. Kundi hili likielewa vizuri nao watakuwa mabalozi wazuri kufikisha ujumbe kupitia kalamu zao," alisema 

Dk Agnes Kijazi. Aidha pamoja na mafunzo hayo, TMA pia ilipokea mrejesho na ushauri kutoka kwa wanahabari ili kuboresha zaidi namna ya utoaji wa taarifa za utabiri wa hali ya hewa kwa umma.  
Picha ya pamoja ya washiriki wa semina kwa baadhi ya waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari juu ya uandishi wa habari za hali ya hewa.

ASKARI WANAWAKE WA JKT MGULANI WAFANYA USAFI WODI YA WAZAZI HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA TEMEKE

 Mkuu wa Idara ya wanawake Wanajeshi wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Kikosi 831 KJ Mgulani (Matron wa Kikosi), Kapteni Lamla Balama baada ya kuzungumza na wanahabari Dar es Salaam leo kuhusu shughuli ya usafi  waliofanya katika Wodi ya Wazazi Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 53 tangu lianzishwe Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),ambayo yatafikia kilele chake kesho nchini.

SABABU YA EID-AL-ADHA KUITWA 'SIKUKUU YA KUCHINJA'


Na Jumia Travel Tanzania

Eid al-Adha ni miongoni mwa sikukuu kubwa kwa waumini wa dini ya Kiislamu ukiachana na Eid- al-Fitr inayosherehekewa kila mwaka duniani kote. Kwa mwaka huu sikukuu hii inatarajiwa kusherehekewa siku ya Ijumaa ya Septemba mosi ambapo kwa waumini wa dini hiyo ni kipindi cha kujitolea, kuonyesha ukarimu kwa marafiki, familia na watu wenye uhitaji.

Kama zilivyo sikukuu nyingine kuna baadhi ya watu huwa hawajui ni kwa nini huwa zinaseherehekewa namna zinavyosherehekewa. Jumia Travel kupitia makala haya imekukusanyia mambo ya msingi kuhusu maana ya sikukuu hii na namna ya kusherehekea.

MAMIA WAMIMINIKA KUJISAJILI KATIKA MFUKO WA FIDIA (WCF) IKIWA UTEKELEZAJI WA AGIZO LA WAZIRI JENISTA MHAGAMA


Meneja Matekelezo  Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, Bw.Victor Luvena, (kulia), akiwahudumia waajiri waliofika kujisajili na kulipa michango leo Agosti 31, 2017.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

MUITIKIO wa waajiri kujisajili na kulipa michango katika Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi (WCF) umekuwa wa kuridhisha hususani Mwezi Agosti, Meneja Matekelezo Bw. Victor Luvena amesema leo Agosti 31, 2017.

Itakumbukwa ya kwamba, tarehe 23 Julai 2017 Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (Mb), alitoa siku 30 kwa waajiri wote nchini ambao walikuwa hawajasajili kuhakikisha wanajisajili katika Mfuko na wanawasilisha michango kwa wakati, vinginevyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao na kama Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi inavyoelekeza.

“Kwakweli tunamshukuru Mheshimiwa Waziri kwa agizo alilolitoa kwani limetoa msukumo mkubwa, waajiri wengi wamejitokeza kutekeleza wajibu wao wa kisheria wa kujisajili na kuwasilisha michango katika Mfuko.” Alisema Bw. Luvena

K-VIS Blog ilishuhudia idadi kubwa ya waajiri wakiwa wamejitokeza leo Agosti 31, 2017 ambayo ndiyo siku ya mwisho kwa waajiri kutekeleza agizo la Mheshimiwa waziri, wakiwa wamejazana kwenye ofisi za WCF  kujisajili na kuwasilisha michango, ambapo kazi hiyo ya kuwahudumia ilikuwa ikiongozwa na Meneja Matekelezo - WCF, Bw.Victor Ruvena.
 Waajiri, wakihudumiwa na maafisa wa WCF, leo Agosti 31, 2017.

 Afisa Matekelezo wa WCF, Bi. Gladness Madembwe, (kulia), akimkabidhi cheti cha usajili Bw.Sultani Ali kutoka kampuni ya Marifas Refregerator ya jijini Dar es Salaam.
 Afisa Matekelezo wa WCF, Bw.Edward Kerenge, (kushoto), akiwahudumia waajiri waliofika kujisajili na Mfuko leo Agosti 31, 2017.
  Afisa Matekelezo wa WCF, Bw.Edward Kerenge, (kulia), akiwahudumia waajiri waliofika kujisajili na Mfuko leo Agosti 31, 2017.
 Afisa Matekelezo Msaidizi wa WCF, Bi.Emiliana J.Gwagilo, akimsikiliza Mwajiri huyu aliyefika kupatiwa huduma leo Agosti 31, 2017.
  Afisa Matekelezo Msaidizi wa WCF, Bi.Emiliana J.Gwagilo, (kushoto), akimuhudumia Mwajiri huyu aliyefika kupatiwa huduma leo Agosti 31, 2017.
  Afisa Matekelezo wa WCF, Bi. Gladness Madembwe,(kushoto), akimuhudumia Bw. Sultani Ali kutoka kampuni ya Marifas Refrigeration, ya jijini Dar es Salaam.
 Meneja Matekelezo  Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, WCF, Bw.Victor Luvena, (kulia), akiwasikiliza waajiri waliofika leo Agosti 31, 2017 ili kupatiwa huduma ya usajili na uwasilishaji michango katika Mfuko huo.
 Maafisa wa WCF (kulia), wakimsikiliza Mama huyu mwajiri aliyefika kupatiwa huduma.



August 30, 2017

Wanataaluma ya Habari Waaswa Kuzingatia Weledi

NAIBU KATIBU MKUU WA CCM BARA AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA CHAMA CHA CPC CHA CHINA

 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM-Bara- Rodrick Mpogolo (kushoto) akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Xu Lyuping (kulia), katika ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM-Bara- Rodrick Mpogolo (wapili kushoto) akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Xu Lyuping (kulia), katika ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa KIanali mstaafu Ngemela Lubinga.
 Ujumbe wa Naibu Katibu Mkuu wa CCM_Bara Rodrick Mpogo na ujumbe wa Naibu Waziri wa mamambo ya Nje wa CPC, wakishangilia baada ya mazungumzo kumalizika. 
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM-Bara- Rodrick Mpogolo akiagana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Xu Lyuping baada ya mazungumzo yao katika ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. (Picha na Bashir Nkoromo).
 Naibu Katibu Mkuu akimsindikiza mgeni wake baada aya mazungumzo hayo
  Naibu Katibu Mkuu akimsindikiza mgeni wake baada aya mazungumzo hayo
  Naibu Katibu Mkuu akimsindikiza mgeni wake baada aya mazungumzo hayo
  Naibu Katibu Mkuu akimsindikiza mgeni wake baada aya mazungumzo hayo
 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM-Bara- Rodrick Mpogolo akiagana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Xu Lyuping baada ya mazungumzo yao katika ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katribu wa NEC Siasa na Uhusian9o wa Kimataifa kanali Mstaafu Ngemela 
 NAIBU Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole akiagana na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Chama Cha Kikomunisti cha China (CPC), Xu Lyuping baada ya mazungumzo hayo
 UGENI HUU SAFI SANA, Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara- Rodrick Mpogolo akimwambia Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Humphrey Polepole baada ya wageni kluondoka baada ya mazungumzo. PICHA NA BASHIR NKOROMO. PICHA NYINGI ZAIDI ZA TUKIO HILO/ BOFYA HAPA

MSHINDI WA SHILINGI MILIONI 30 YA DROO YA JUMAPILI YA JACKPOT YA TATU MZUKA AKABIDHIWA FEDHA ZAKE

 Balozi wa Mchezo wa Tatu Mzuka, Mussa Hussein (kushoto), akimkabidhi hundi ya shilingi milioni 30 mshindi wa droo ya Jumapili ya Jackpot ya Tatu Mzuka, Tausi Mashombo jijini Dar es Salaam jana, aliyojishindia kutoka katika mchezo wa Tatu Mzuka ambao umejizolea umaarufu kwa kutoa washindi kila saa. Jackpot hiyo inaendelea Jumapili hii kwa mshindi kujishindia shilingi milioni 80.

August 28, 2017

NIC Bank yakabidhi magari Matatu kati ya Sita Kwa Mteja wake kama Mkopo

Meneja mahusiano kwa wateja wakubwa wa benki ya NIC Tanzania, Woinde Murro(kulia) akizungumza jambo na mmoja wa wateja waliofika kwaajili ya kukabidhiwa magari makubwa ikiwa awamu ya kwanza ya mkopo wa Magari Sita ambapo leo amepokea magari matatu na matela matatu
Meneja mahusiano kwa wateja wakubwa wa benki ya NIC Tanzania, Woinde Murro(kulia) akimkabidhi funguo  Mkurugenzi wa kampuni ya Usafirishaji ya Simeta, Bw.Zainul Dossa(kushoto) za magari matatu waliyokopeshwa na Benki ya NIC
Meneja Uendeshaji kutoka Kampuni ya Usafirishaji ya Simera, Bw. Arif akiwasha moja ya gari mara baada ya Benki ya NIC kukopesha magari sita kwenye kampuni ya Usafirishaji ya Simera leo jijini Dar es Salaam.
Magari matatu kati ya sita yalikabidhiwa na benki ya NIC kama mkopo kwa mteja wao.

Leo benki ya NIC imekabidhi magari makubwa matatu na matela yake kati ya magari sita ambayo yamekabidhiwa kama mkopo kwa Mteja wao Simera. Makabidhiano ya Magari hayo yamefanyika katika Ofisi za FAW zilizopo Barabara ya Nyerere jijini Dar Es Salaam.

Mkurugenzi wa kampuni ya Usafirishaji ya Simera, Bw.Zainul Dossa amepokea magari hayo kati ya sita waliyokopeshwa na Benki ya NIC mapema leo huku magari mengine matatu yatakabidhiwa hivi karibuni.

MAHAFALI YA 6 YA GENIUS KINGS YAFANA JIJINI DAR

Mkurugenzi Mkuu wa Shule ya Genius Kings Nusery& Primary School, Machage Kisyeri, (Kulia) akisoma hotuba.
Mwalimu Mkuu wa shule, Aloyce Siame (kushoto) akimkabidhi risala Profesa Joseph Kahamba , ambaye alikuwa mageni rasmi wakati wa mahafali hayo.Katikati ni Mkurugenzi wa shule Julius Rutabanja.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Aloyce Siame (kulia) akikabidhiwa zawadi ya kikombe na Profesa Joseph Kahamba.
Paroko msaidizi wa Roho Mtakatifu Parokia ya Segerea Velence Kisaka (kulia) akibarikia shule hiyo baada ya kufanya ibada kwa ajili ya kuwaombea wanafunzi wa darasa la saba wanaojiandaa na mitihani ya taifa.
Mwalimu wa Dini ya Kiislam Shekhe Hussein Abdalah akiongoza swala kwa ajili kawaombea watoto wa darasa la saba katika shule hiyo.
Mgeni rasmi akiangalia wanafunzi wakifanya majaribio ya sayansi.
Wahitimu wakitoa burudani kwa wazazi na wageni waalikwa.
Kikosi cha scout shuleni hapo wakifanya mambo yao
Wanafunzi wakionyesha kipaji cha kucheza ngoma za asili.


*Wahitimu waaswa kwenda na kasi ya sayansi na teknolojia
Wakati serikali ya Tanzania inao mkakati wa kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda,wanafunzi wanaohitimu masomo wametakiwa kujiona sehemu ya mkakati huo na kusoma kwa bidii kupata ujuzi wa taaluma mbalimbali ikiwemo kutoogopa kusoma masomo ya hesabu na sayansi.

Ushauri huo umetolewa na daktari bingwa nchini wa magonjwa ya nevu (Neurosurgery) kutoka Chuo Kikuu cha Muhimbili,Profesa Joseph Kahamba, wakati wa mahafali ya darasa la saba ya msingi ya Genius Kings yaliyofanyika Segerea jijini Dar es Salaam .

Profesa Kahamba alisema kuwa nchi yetu bado inakabiliwa na changamoto ya kuwa na wataalamu waliobobea katika nyanja mbalimbali ambapo aliwataka wanafunzi wanaohitimu masomo na waliopo mashuleni na vyuoni kujipanga kuhakikisha wanapata utaalamu wa fani mbalimbali tayari kwa kutumikia taifa la Tanzania.
“Wanafunzi waliopo mashuleni na vyuoni mnapaswa kujipanga kwa kuhakikisha mnasoma kwa bidii na kupata ujuzi wa fani mbalimbali kwa kuwa mapinduzi ya kuendeleza taifa letu yanayoendelea yanahitaji wataalamu wa fani mbalimbali na wanaotegemewa kuchukua majukumu hayo hawatoki nje ya nchi bali ni nyinyi vijana wa kitanzania”Alisema Profesa Kahamba.

Aliongeza kusema kuwa kinachotakiwa kwa wanafunzi waliopo mashuleni na vyuoni kujibidisha kusoma kwa bidii na kupata taaluma za fani mbalimbali na wahakikishe wanajiamini na kuhakikisha ndoto zao walizojiwekea zinatimia na wanakuwa na uzalendo wa kuitumikia nchi na kuleta maendeleo chanya katika jamii kupitia elimu waliyoipata.

Profesa Kahamba aliupongeza uongozi wa shule ya Genius Kings kwa kufanya uwekezaji katika sekta ya elimu kwa kuwa umelenga kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha elimu nchini na kuleta mabadiliko wenye jamii kwa kuwa elimu ni njia pekee ya kuleta maendeleo kwa haraka katika ujenzi wa taifa . “Naupongeza uongozi wa shule kwa kuwekeza katika elimu na nawapongeza wazazi ambao wanawekeza katika elimu kwa kusomesha watoto wao maana elimu bora katika jamii inachangia kuleta mabadiliko ya nchi haraka”.Alisema

Mwalimu Mkuu wa shule hiyo Bw. Aloyce Siame, alisema kuwa katika kipindi cha miaka 10 tangu shule ianzishwe imeweza kushikilia rekodi ya kufanya vizuri kwa kufaulisha wanafunzi wa darasa la saba na la nne kwa kiwango cha juu na kuingia katika shule tano bora wilayani Ilala na shule bora 20 mkoani Dar es Salaam mfululizo hali ambayo imewajengea hari ya kuzidi kufanya vizuri kwa mwaka huu na miaka ijayo.

“Moja ya mtazamo wa shule hii ni kuifanya kuwa shule bora ya mfano inayotoa elimu bora nchini kuanzia shule ya awali na shule ya msingi na sekondari.”Tumejipanga kuhakikisha lengo hili linatimia na tunatoa shukrani kwa serikali,wazazi na wadau wote ambao wameonyesha kutuunga mkono katika kipindi hiki cha awamu ya kwanza ya mwanzo ya miaka 10 na kuwezesha mafanikio haya kupatikana”.Alisema.

Kwa upande wake,Mkurugenzi mkuu wa shule hiyo ,Bw.Machage Kisyeri,aliwapongeza wahitimu kwa kufikia hatua hiyo na aliwataka watumie elimu waliyoipata kujipanga zaidi kwa masomo ya sekondari ambayo yanawakabili mbele yao. “Maisha sio lelemama mnapaswa kupambana zaidi katika hatua inayofuatia na kuhakikisha msingi wa elimu imara tuliyowapatia unawaongoza kuelekea katika kupata mafanikio ya kitaaluma popote pale mtakapokwenda”Alisisitiza.

Aliongeza kuwa shule imejizatiti kuunga mkono jitihada za serikali za kuboresha elimu nchini ambapo kuanzia mwezi Januari mwakani itaanza kutoa elimu ya sekondari katika shule yake mpya iliyojengwa sehemu ya Mataya wilayani Bagamoyo katika mkoa wa Pwani.
Kuhusiana na changamoto wanazokabiliana nazo alisema kuwa zipo changamoto za kawaida kinachotakiwa ni ushirikiano baina ya wazazi,walimu,na wadau wanaosimamia elimu ili kuhakikisha mafanikio yanapatikana na elimu ya Tanzania inazidi kupanda “Walimu wakiwezeshwa vizuri na kupewa ushirikiano wa kutosha naamini shule nyingi za Tanzania zitatoa elimu bora kwa kuwa tunao walimu wengi wazuri ambao wakitumiwa ipasavyo tutasonga mbele”.Alisema.

August 26, 2017

DKT. MWINUKA AWAPONGEZA WAHANDISI WANAWAKE TANESCO, KWA KUPEWA TUZO

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka, (kushoto), akipokea kikombe (tuzo), kutoka kwa Mwakilishi wa Wahandisi wanawake kutoka Shirika hilo, Mhandisi Rosamystica Lutenganya, katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya Shirika hilo jijini Dar es Salaam Agosti 25, 2017. Wahandisi wanawake wa TANESCO walikabidhiwa tuzo hiyo na Makamu wa Rais, baada ya kuibuka  wa kwanza kwenye kongamano na maonesho linalowakutanisha wahandisi wanawake kutoka sekta mbalimbali hapa nchini lijulikanalo kama "Tanzania Women Engineers Convention and Exhibition-TW=AWECE". Wahandisi hao walionesha umahiri mkubwa jinsi wanavyoweza kutumia teknolojia ya kisasa katika usimamizi wa miundombinu ya usambazaji umeme (Distribution Control Centre) inayotumika kuboresha huduma.

NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka, (pichani), amewataka Wahandisi Wanawake wa Shirika hilo, kutembelea mashuleni ili kuwahamasisha (Motivate), wanafunzi wa kike ili wapende kujisomea masomo ya sayansi na Hisabati na hatimaye baadaye waje kushika nafasi kama walizo nazo wao.

Dkt. Mwinuka ameyasema hayo makao makuu ya TANESCO jijini Dar es Salaam, wakati akiwapongeza Wahandisi wanawake wa Shirika hilo, baada ya kupewa tuzo na Makamu nwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa kuibuka wakwanza kwenye Kongamano la Wahandisi wanawake Tanzania “Tanzania Women Engineers Convention and Exhibition, (TAWECE), ambalo huenda sambamba na maonesho ya shughuli za kihandisi lililofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

“Niwapongeze sana kwa kuibuka washindi wa kwanza kwenye maonesho hayo, lakini niwaase, mpatapo nafasi mtembelee mashuleni ili muwahamasishe wanafunzi wasichana kupenda kusoma masomo ya sayansi na hisabati, na kwa kupitia kwenu, wanaweza kujitokeza wasichana wengi kupenda masomo hayo na hivyo baadaye kufanya kazi za kihandisi kama nyinyi.” Alisema Dkt. Mwinuka.

Dkt. Mwinuka alisema, tuzo hiyo ni heshima kubwa kwa Shirika kwani inajenga picha (image) nzuri mbele ya jamii kuonyesha juhudi zetu za kuwahudumia wateja wetu. Alisema.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake kwenye hafla hiyo fupi, Mhandisi Rosamystica Lutenganya, alisema Wahandisi wanawake kutoka TANESCO, walionyesha umahiri wao katika kuelezea teknolojia ya usimamizi wa miundombinu ya usambazaji umeme (Distribution Control Centre), inayotumia kuboresha huduma wanazozitoa katika jamii.

“Lakini pia si hivyo tu, tulionyesha uboreshaji wa huduma tunazozitoa kwa wateja kwa kutumia teknolojia ya kisasa kupitia mfumo wa fiber ambao upitishaji taarifa mbalimbali kama vile mawasiliano na picha na hii inawezesha mfumo kuliona tatizo la mteja mara tu linapotokea na kuwezesha TANESCO kuchukua hatua haraka bila mteja kupata usumbufu.” Alisema Mhandisi Lutenganya.

Katika Kongamano hilo la mwaka huu lililofanyika Julai 28, (2017), kulikuwa na makundi matatu ya washiriki, ambayo ni shule za Sekondari, taasisi za elimu ya juu na mashirika ya umma ambapo waandaaji waliangalia uandaaji, uelewa wa washiriki pamoja na teknolojia ilivyotumika.

TANESCO ina wahandisi wanawake 55, na kuifanya taasisi ya kwanza nchini kuwa na idadi kubwa na wahandisi wanawake.

Naye Naibu Mkurugenzi Mtendaji waTANESCO (anayeshughulikia usambazaji na huduma kwa wateja), Mhandisi Joyce Ngahyoma, alisema ni wajibu wa wanawake kujiamini katika utekelezaji wa majukumu yao na kuachana na dhana ya woga.
“Fanyeni kazi kwa bidii na maarifa, na niwaambie, utendaji kazi wako ndio utamvutia MD afikie uamuzi wa kukupandisha cheo na sio jambo linguine lolote lile, mimi nitastaafu hivi karibuni, ninawaeleza haya kwavile ninajua umuhimu wa kujituma katika kazi na kujiamini.” Alisema Mhandisi Ngahyoma.

Alionyesha kufurahishwa kwake, na angependa idadi ya wanawake viongozi katika Shirika hilo inaongezeka na kufikia sio asilimia 50 tu bali asilimia 75.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji waTANESCO (anayeshughulikia usambazaji na huduma kwa wateja), Mhandisi Joyce Ngahyoma, akiwa na Dkt. Mwinuka wakati akionyesha tuzo hiyo.

 Dkt. Mwinuka, akiwapongeza baadhi ya wahandisi hao.
 Dkt. Mwinuka akizungumza wakati wa hafla hiyo.
 Naibu Mkurugenzi Mtendaji waTANESCO (anayeshughulikia usambazaji na huduma kwa wateja), Mhandisi Joyce Ngahyoma, akitoa nasaha zake.
 Mwakilishi wa Wahandisi wanawake kutoka Shirika hilo, Mhandisi Rosamystica Lutenganya, akizungumza.

 Naibu Mkurugenzi Mtendaji waTANESCO (anayeshughulikia usambazaji na huduma kwa wateja), Mhandisi Joyce Ngahyoma, akitoa nasaha zake.
 Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
  Kaimu Meneja Uhusiano wa TANESCO, Bi. Leila Muhaji, akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Picha ya pamoja.