Afisa Matukio
wa Airtel Dangio Kaniki (kulia) akimuonyesha applikesheni ya
VSOMO Mkuu wa Usajili Veta Kipawa (Registry) Bw, Harold
Mganga (katikati) pamoja na Mratibu wa Miradi na Kozi fupi.
(Project and Short Course Coordinator) Veta Kipaw bw, Gosbert Kakiziba
(kulia). hafla fupi ya makabidhiano ya simu hizo yaliyofanyika Veta
Kipawa. Aplikesheni ya VSOMO inatoa mafunzo ya ufundi stadi ya VETA kwa njia ya
mtandao inayodhaminiwa na Airtel Tanzania.
XXXXXXXXXXXXXXX
DAR ES SALAAM
Mamlaka ya elimu ya ufundi Tanzania
(VETA) kwa kupitia mfumo wa mafunzo kwa mtandao wa VSOMO unaodhaminiwa na
kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imebainisha kuwa iko tayari kuhudumia
vikundi au jamii ya wanaotaka kujifunza ufundi stadi kwa kupeleka timu yao ya
mafunzo kwa vitendo popote ili kuhakikisha dhana ya uchumi wa viwanda
inakamilika kwa kuwa na mafundi wazuri waliohitimu ufundi katika chuo maalumu
nchini.
Hayo yamebainishwa na mkuu wa chuo cha
Veta Kipawa ambae pia ni msimamizi wa mradi wa mafunzo kwa njia ya simu
unaodhaminiwa a Airtel kwa lengo la kutoa FURSA kwa vijana wegi mjini kupata
ujuzi na kujiajiri Mhandisi Lucius Luteganya.
“VETA tuko tayari kuwafuata wanafunzi
wetu endapo watajiandikisha na kuhamasihana kwa kikundi kusoma kwa njia
ya mtandao wa VSOMO , ikiwa watakuwa vijana kuanzia 15-20 na wakipenda kupata
mafunzo waliko basi sisi tutawafuata waliko ili kuhakikisha wanahudumiwa
na mobile trainers wetu”
“sasa hivi kupitia mtandao wa Vsomo
tunakozi 12, wanafunzi wanaweza wakajisomea wawapo popote mara baada ya kupakua
App yetu ya VSOMO na kulipia kozi anayotaka” alisisitiza Luteganya
Eng Luteganja alitaja kozi hizo kuwa ni
“Tunampango waongeza kozi zingine 15 hivi karibuni lakini kwa sasa
zilizopo tayari kwenye mtandao ni Huduma ya chakula na mbinu za kuhudumia
wateja, Matengenezo ya kompyuta, umeme wa viwandani, ufundi Bomba wa Majumbani
, Umeme wa magari, Ufundi umeme wa manyumbani, Ufundi pikipiki, Ufundi wa simu
za mkononi, Ufundi Alluminium, Utaalamu wa maswala ya urembo pamoja ma
Ufundi wa kuchomea vyuma.
Tangu VETA na Airtel walipozindua
mfumo huu wa mafunzo kwa njia ya mtandao waVSOMO mwezi wa Juni 2016 Mfumo huu
wa VSOMO sasani umepata umaarufu mkubwa kwa vijana ambapo takwimu zinaonyesha
zaidi ya vijana 30,000 tayari wamepakua application ya VSOMO, 8000
wamejiandikisha na kati yao 50 wameshasoma kozi mbalimbali na kupata
vyeti vyao vya ufundi stadi kutoka VETA.
kujiandikisha katika mojawapo ya kozi
12 zinazopatikana katika application ya VSOMO mwanafunzi atalipia kwa simu yake
gharama ndogo ya shilingi 120,000 tu kupitia huduma ya Airtel Money kwa kupiga
*150*60#. na kufanya malipo ambazo gharama hizi zitamuwezesha kuja kupata
mafunzo kwa vitendo bila malipo ya ziada.
No comments:
Post a Comment