Meneja
Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando akiongea na mmoja kati ya
washidi wakati Airtel Ilipochezesha droo ya SHINDA
NA SMATIKA intaneti ambapo washindi 2000 kila mmoja alijishindia 1GB.
Kushoto ni ni Afisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania Abdallah
Hemedy na Afisa Masoko Airtel Nassoro Abubakar.
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
DAR ES
SALAAM
Kampuni ya simu za mkokoni Airtel
Tanzania leo imewazadia washindi 2,000 wa kwanza wa promosheni ya SHINDA NA SMATIKA Intaneti kwenye droo ambayo imechezesha
jijini Dar es Salaam.
Promosheni
ya SHINDA
NA SMATIKA Intaneti ilizunduliwa
mapema wiki hii ambapo kuna washindi 1,000 wakila siku ambao wanajishindia
bando ya 1GB pamoja na zawadi nyingine zikiwepo wakishinda simu za kisasa za
smatiphone na moden.
Akiongea
baada ya droo hiyo, Meneja Uhusiani Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema
wateja wa Airtel 2000 wameweza kujishindia bando ya 1GB.
Kama
mnvyoona hapa leo droo ya promosheni yetu ya SHINDA
NA SMATIKAIntaneti inafanyika kwa uwazi kabisa na washindi. Ni ya
promosheni hii ni kutoa shukrani kwa wateja wa Airtel kwa kuonyesha uaminifu
wao kwa kuendelea kutumia mtandao bora kabisa hapa nchini, alisema Mmbando.
Ni muhimu kufahamu kuwa mteja haitaji kujisajili kwa ajili ya
promosheni ya SHINDA NA SMATIKA
Intaneti. Kile anachotakiwa kufanya ni kupiga *149*99# halafu changua namba 5 Yatosha SMATIKA Intaneti, hapo
atanunua bando aidha ya siku, wiki au mwezi na kuwa mmoja wa washindi wa zawadi
zetu kambambe, alisema Mmbando.
Mmbando
aliongeza kuwa promosheni ya Shinda na Yatosha
SMATIKA intaneti ilizinduliwa mwanzo mwa wiki na itakuwa ni ya siku 30
huku kukiwa na droo 3 kila wiki – Jumatatu, Jumatano na Ijumaa. Kwa droo za
kila siku, wateja 1000 watajishindia bando ya intaneti yenye 1GB kila mmoja
wakati kwenye droo kubwa kutakuwa na washindi 10 huku watano wakishinda simu za
smatiphone na 5 wakijishindia moden.
No comments:
Post a Comment