Na Hamza Temba, WMU, Muheza Tanga
..........................................................................
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ameuagiza uongozi wa Wakala wa
Huduma za Misitu Tanzania TFS kujenga kituo cha ulinzi cha kudumu katika eneo
la chanzo cha maji ya mto zigi kilichopo ndani ya Hifadhi ya Mazingira Asilia
Amani kwa ajili ya kulinda chanzo hicho.
Dk.
Kigwangalla ametoa agizo hilo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea eneo la chanzo hicho na
kukuta uharibifu mkubwa unaofanywa na baadhi ya wananchi wanaodaiwa kuchimba
madini ya dhahabu katika eneo hilo la hifadhi kinyume cha sheria
"Nimeagiza
watu wa TFS wajenge kituo cha ulinzi cha kudumu katika eneo hili, na waweke
walinzi wetu wa kudumu hapa badala ya kutegemea kufanya patrol (doria) na kuondoka,
kwasababu eneo hili wananchi wanaamini lina madini ya dhahabu kwahivo kila siku
wataendelea kuja kujaribu kuvuna dhahabu kutoka hapa.
"Kwasababu
sisi kazi yetu ni kuhifadhi Maliasili ambayo tumepata kama urithi wa nchi yetu,
niwahakikishie kwamba tutaimarisha ulinzi kwa kuanzisha kituo cha ulinzi hapa
ili askari wawe wanabadilishana na kudhibiti kabisa uharibu ambao umekuwa
ukifanyika, kwasababu maji yanayotoka katika chanzo hiki yanakwenda kunywesha
Muheza yenyewe na wilaya wa Tanga, tukiharibu hapa yatakosekana maji safi na
salama" alisema Dk. Kigwangalla.
Kwa
upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala huyo, Prof. Dos Santos Silayo alisema
pamoja na eneo hilo kwa sasa kuwa linalindwa na askari wa Suma JKT
watahakikisha ulinzi unakuwepo muda wote kwa kutekeleza agizo hilo la Waziri la
kujenga kituo cha ulinzi cha kudumu ili askari wawepo katika eneo hilo muda
wote.
"Lengo
letu ni kuhakikisha kwamba wananchi hawaingii ili tusiwe tunawashtukiza
kuwakamata na kwachukulia hatua, lazima tuwe watu wa kuzuia uhalifu usitokee,
nia yetu ni kuwa na kituo mara moja kama alivyoelekeza Mhe. Waziri na hili
jambo tumelichukua kama maelekezo na tutalitekeleza kwa nguvu kabisa,"
alisema Prof. Dos Santos Silayo.
Awali
Dk. Kigwangalla alitembelea kikundi cha wafugaji wa vipepeo katika Tarafa ya
Amani ambao waliiomba Serikali ifungulie vibali vya kusafirisha bidhaa hiyo nje
ya nchi, aliahidi kuyafanyia kazi maombi yao huku akiwataka kutumia fursa ya
ufugaji huo kama bidhaa ya utalii kuwavutia watalii wanaotembelea Hifadhi ya
Mazingira Asilia Amani.
Akiwa
mkoani Tanga alitembelea pia Kituo cha Mambo ya Kale cha Mapango ya Amboni na
kusema Wizara yake itaboresha kituo hicho pamoja na vituo vingine vya Mambo ya
Kale ili kupanua wigo wa vivutio vya utalii nchini viweze kuchangia zaidi
kwenye pato la Taifa.
Katika
ziara hiyo ya siku moja mkoani Tanga alitembelea pia shamba la miti ya Mitiki
Longuza, Makumbusho ya Shaban Robert na Hifadhi ya Taifa ya Mkomazi.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiangalia vipepeo katika moja
shamba la wafugaji katika Tarafa ya Amani Jijini Tanga jana. Mbali na biashara
ya kuuza vipepeo hao nje ya nchi aliwataka wafugaji hao kutumia fursa ya
ufugaji huo kama bidhaa ya utalii kwa kuandaa maonesho maalum ya kuwavutia
watalii wanaotembelea Hifadhi ya Mazingira Asilia Amani
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipokea zawadi ya pambo la
vipepeo kutoka kwa mmoja wa wafugaji Asina Athumani muda mfupi baada ya kukagua
shamba la vipepeo katika Tarafa ya Amani Jijini Tanga jana ambapo aliwataka
wafugaji hao kutumia fursa ya ufugaji huo kama bidhaa ya utalii kwa kuandaa
maonesho maalum ya kuwavutia watalii wanaotembelea Hifadhi ya Mazingira Asilia.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisaidia baadhi ya watu kupanda
mlima baada ya kukagua chanzo cha maji cha Mto Zigi ambacho kipo ndani ya
Hifadhi ya Mazingira Asilia Amani wilayani Muheza mkoa wa Tanga. Ameiagiza TFS
kujenga kituo cha ulinzi cha kudumu katika eneo hilo linalovamiwa na wananchi
kwa madai ya kuchimba madini ya dhahabu.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akikagua moja ya shamba la vipepeo
katika Tarafa ya Amani Jijini Tanga jana ambapo aliwataka wafugaji hao kutumia
fursa ya ufugaji huo kama bidhaa ya utalii kwa kuandaa maonesho maalum ya kuwavutia
watalii wanaotembelea Hifadhi ya Mazingira Asilia Amani tofauti na hivi sasa
wanapotegemea soko la kuuza nje ya nchi. Kulia ni Mbunge wa Muheza, Balozi Adadi
Rajabu.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mhifadhi Mkuu wa
Kituo cha Mapango ya Amboni, Jumanne Gekora kukagua kituo hicho jana
Jijini Tanga ambapo alisema Serikali itaboresha kituo hicho pamoja na vituo
vingine vya Mambo ya Kale ili vichangie zaidi kwenye pato la Taifa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mhifadhi Mkuu wa Kituo cha Mapango ya Amboni, Jumanne Gekora kukagua kituo hicho jana Jijini Tanga ambapo alisema Serikali itaboresha kituo hicho pamoja na vituo vingine vya Mambo ya Kale ili vichangie zaidi kwenye pato la Taifa.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozwa na Mhifadhi Mkuu wa Kituo cha Mapango ya Amboni, Jumanne Gekora kukagua kituo hicho jana Jijini Tanga ambapo alisema Serikali itaboresha kituo hicho pamoja na vituo vingine vya Mambo ya Kale ili vichangie zaidi kwenye pato la Taifa.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa Mhifadhi
Mkuu wa Kituo cha Mapango ya Amboni, Jumanne Gekora kuhusu kivutio cha
utalii cha umbo la asili la ramani ya Afrika alipotembelea mapango hayo jana
Jijini Tanga.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo kutoka kwa
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo
kuhusu asali inayozalishwa na Wakala huyo kupitia shamba la Miti Sao Hill muda
mfupi kabla ya kuikabidhi kwa Asha Shaban ambaye ni dada yake na aliyekuwa
mshairi na mwandishi mashuhuri wa riwaya Shaban Robert alipotembelea makumbusho
ya mwandishi huyo Jijini Tanga jana.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi Asha Shaban ambaye
ni dada yake na Shaban Robert aliyekuwa mshairi na mwandishi mashuhuri wa
riwaya zawadi ya asali inayozalishwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania TFS
kupitia shamba la Miti Sao Hill alipotembelea makumbusho ya mwandishi huyo
Jijini Tanga jana.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiongozana na Mtendaji Mkuu wa
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania, Prof. Dos Santos Silayo kukagua Kituo cha Mapango
ya Amboni wakati wa ziara yake ya kikazi Jijini Tanga jana ambapo alisema
Serikali itaboresha kituo hicho pamoja na vituo vingine vya Mambo ya Kale ili
vichangie zaidi kwenye pato la Taifa.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipata maelezo ya namna ya
kupanda miti ya Mitiki kutoka Meneja wa shamba la Miti Longuza alipotembelea
shamba hilo jana wilayani Muheza Mkoani Tanga.
No comments:
Post a Comment