NA K-VIS BLOG/Khalfan
Said, MOSHI
MADAKTARI na
watoa huduma kutoka Kanda ya Kaskazini, waliokuwa wakishiriki mafunzo ya siku
tano (5), ya kufanya tathmini ya mfanyaakzi aliyepata ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo
na kazi amesema wamepata nyezo muhimu itakayowasaidia kutekeleza
majukumu hayo kwa usahihi na haraka.
Akizungumza kwa
niaba ya washiriki wenzake wakati wa kufunga mafunzo hayo yaliyokuwa
yakifanyika mjini Moshi, Februari 23, 2018, Dkt. Peter Mabula kutoka Arusha
Lutheran Medical Centre alisema, wengi wao walikuwa hawafahamu nini cha kufanya
wanapomuhudumia mfanyakazi aliyepata madhara yatokanayo na kazi, ili kumfanyia
tathmini kwa ajili ya kulipwa Fidia stahiki bali walitumia uwezo wao wa kawaida
wa kidaktari.
“Mafunzo yametuwezesha
ni jinsi gani daktari utafanya tathmini na ukadiriaji wa matatizo mbalimbali
yatokanayo na kazi mbalimbali aliyopata mfanyakazi, kuelewa mgonjwa wa aina fulani
anapofika kupatiwa huduma utamuhudumia kwa kutumia vigezo vilivyopo kisheria,
lakini pia usahihi wa kujaza takwimu zake katika kumbukumbu za kitabibu.” Alisema.
Akizungumza
kwa niaba ya Mkuu wa wilaya ya Moshi, Katibu Tawala Msaidizi wa Manispaa hiyo, Bw. Sebastian
Masanja
Aliupongeza
Mfuko kwa kuandaa mafunzo hayo kani yatawezesha kuwepo na madaktari ambao
wamepatiwa mafunzo maalum ya kufanya tathmini ili kutoa fidia inayostahili.
“Tulikotoka
jamani hatukuwa na utaratibu maalum unaoeleweka kwamba ukiumia kazini unaenda
kumuona nani na huyo mtu unaeenda kumuona hujui ni lini atakufidia kulingana na
ulemavu ulioupata.” Alisema Bw. Masanja.
Lakini
pia, aliwaasa madaktari na watoa huduma hao, kutumia elimu waliyopata ili kutoa
tathmini sahihi na hatimaye mgonjwa aliyeumia aweze kupata haki stahiki na kwa
haraka.
Naye Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, wa
Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), ambao ndio waandaaji wa mafunzo hayo,
Dkt. Abdulsalaam Omar alisema, jumla ya washiriki 66 kutoka mikoa ya
Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Tanga walishiriki mafunzo hayo, chini ya
wataalamu wa WCF na wawezeshaji waliobobea kwenye maswala ya usalama mahala pa
kazi kutoka taasisi ya Mifupa MOI.
Alisema mafunzo haya ni
mundelezo wa mafunzo kama haya ambayo yamekuwa yakifanyika kwa awamu kwenye
kanda mbalimbali nchini, ili kujenga mtandao wa wataalamu wa kufanya tathmini ya
ulemavu uliotokana na ajali au magonjwa yatokanayo na kazi kwa mujibu wa
mkataba.
“
Idadi ya madaktari ambao wamepatiwa mafunzo haya nchi nzima hadi sasa ni 655 na tunatarajia kutoa mafunzo zaidi ili wafanyakazi
waweze kupata huduma kwa ukaribu lakini kwa haraka na usahihi.” Alifafanua Dkt.
Abdulsalaam.
Katibu Tawala Msaidizi wa Manispaa hiyo, Bw. Sebastian Masanja, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Moshi, akitoa hotuba ya kufunga mafunzo hayo |
Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, wa
Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), ambao ndio waandaaji wa mafunzo hayo,
Dkt. Abdulsalaam Omar, akizungumza.
Bi. Naanjela S.Msangi, Meneja tathmini ya hatari mahala pa kazi wa WCF, (mbele), akiwa na washiriki |
Dkt. Peter Mabula kutoka Arusha Lutheran Medical Centre, akizungumza kwa niaba ya washiriki wenzake
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, WCF, Bi. Laura Kunenge, akionyesha stika hizo za utambuzi wa ofisi ya mtoa huduma ya tathmini.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, WCF, Bi. Laura Kunenge, akimkabidhi stika ya utambuzi wa ofisi ya mtoa huduma ya tathmini, DktJosephine Rogate, kutoka Hospitali ya Mawenzi.
Mmoja wa washiriki Dkt. Theresia Temu
Mgeni rasmi, Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Kilimanjaro, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Bw. Sebastian Masanja, akimkabidhi cheti Dkt. Theresia Temu, cha ushiriki wa mafunzo ya siku tano ya kufanya tathmini ya mfanyaakzi aliyepata ulemavu uliotokana na ajali na magonjwa yatokanayo
na kazi, yaliyowaleta pamoja madaktari 66 kutoka mikoa ya Kaskazini,
Baadhi ya washiriki
Meneja
tathmini ya madai, (Claims Assessment Manager), wa Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Ali Mtulia, akitoa mada ya namna ya kufanya tathmini
na ukadiriaji(Assessment and evaluation)
Meneja
tathmini ya madai, (Claims Assessment Manager), wa Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Ali Mtulia, akitoa mada ya namna ya kufanya tathmini
na ukadiriaji(Assessment and evaluation)
|
Meneja
tathmini ya madai, (Claims Assessment Manager), wa Mfuko wa Fidia kwa
Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Ali Mtulia, akitoa mada ya namna ya kufanya tathmini
na ukadiriaji(Assessment and evaluation)
Daktari bingwa wa uchunghuzi wa vijidudu na madawa,(Medical Microbiology and
Immunology), Profesa John Shao, (kulia), akiteta jambo na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, wa
Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar.
Daktari bingwa wa uchunghuzi wa vijidudu na madawa,(Medical Microbiology and
Immunology), Profesa John Shao, (kulia), akipongezwa na Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Tathmini, wa
Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), Dkt. Abdulsalaam Omar, kwa kuwapa uzoefu wake wa kazi katika sekta ya afya na tiba washiriki hao.
Profesa Shao, (kulia), akiagana na Katibu Tawala Msaidizi wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Sebastian Masanja baada ya kufungwa kwa mafunzo hayo.
Profesa Shao, (kushoto), akibadilishana mawazo na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano, WCF, Bi.Laura Kunenge, katikati), na Bi. Naanjela S.Msangi, Meneja tathmini ya hatari mahala pa kazi
Wawezeshaji (watoa mada), kutoka kushoto, Dkt. Hussein, Dkt. Mshashu na Dkt. Mhina.
Afusa mwandamizi kutoka WCF, Dkt. Pascal Magesa, akigawa fomu za tathmini ya mafunzo |
Picha ya kwanza ya pamoja
Picha ya pili ya pamoja |
No comments:
Post a Comment