Na Humphrey
Shao, Globu Ya jamii
Waziri wa
Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage anataraji kufungua kongamano
kuhusu Maendeleo ya Viwanda Tanzania
litakalo fanyika katika chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere February 23 Mwaka huu.
Akizungumza na
Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam leo
Afisa Habari wa chuo Hicho
Evelyn Mpasha amesema kuwa Kongamano hilo
kubwa litawaleta karibu wadau mbalimbali wa masuala ya maendeleo ya Viwanda
nchini.
“Kongamano
hili litaangazia Masuala ya Maendeleo ya Uchumi , Uwekezaji Endelevu katika Viwanda, Ujasiliamali katika Uwekezaji
katika Viwanda kwa mfumo wa ushirikiano kati ya sekta ya Umma na sekta binafsi”
amesema Mpasha.
Kwa upoande mmoja wa watoa mada katika
kongamano hilo Binto Mawazo amesema kongamano hili ni sehemu ya juhudi za chuo
kushiriki katika kuunga mkono juhudi za serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania katika kuipeleka Tanzania katika uchumi wa Viwanda .
Binto amesema kuwa MNMA kama chuo ni wadau
Muhimu sana katika kukiwezesha wananchi kufika malengo ya Rais kuipeleka nchi katika
uchumi wa kati.
No comments:
Post a Comment