Tangazo

March 12, 2018

AIRTEL YAENDELEA KUSOGEZA HUDUMA ZA AIRTEL MONEY KARIBU KATIKA MIKOA MBALIMBALI

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Mama Mary Tesha (katikati aliyeshika mkasi) akiwa pamoja na Meneja Miradi ya Airtel Kanda ya Ziwa Joseph Mushi (mwenye tshirt nyekundu) pamoja na wadau wengine muhimu tayari kukata utepe ili kuzindua duka la Wakala wa huduma za  kampuni ya simu za Mkononi ya Airtel,eneo la Nyegezi, jirani na kituo cha mabasi yaendayo maeneo mbalimbali nchini.
 Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Mama Mary Tesha (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Meneja Miradi ya Airtel Kanda ya Ziwa Joseph Mushi
XXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXXX

MWANZA

Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Mkoani Mwanza Mama Mary Tesha ameipongeza Artel Tanzania kwa juhudi zake za kupeleka huduma kwa wateja huku pia akitoa onyo kwa Mawakala wa Mitandao ya simu kuacha hila na udanganyifu kwa wateja ili kujenga imani ya mitandao hiyo kwa Jamii.

Bi Tesha amebainisha hayo wakati akifungua moja ya maduka ya kisasa ya kutolea huduma ya kampuni ya simu za Mkononi ya Airtel eneo la Nyegezi,jirani na kituo cha mabasi yaendayo maeneo mbalimbali nchini.

“Wananchi wetu wamelizwa sana kutokana na mawakala kutokuwa waamifu na waadilifu,Ukweli Serikali haitawafumbia machi kuona wananchi wanaibiwa” …Alisema Mama Tesha

Mama Tesha amewaomba wananchi wa kata 18 za wilaya ya Nyamagana kuyatumia maduka yanayofunguliwa na Airtel kupata huduma za ukakika zilizosogezwa katika maeneo yao na kuwafichua mawakala wasio waaminifu.

Aidha amewaomba wananchi kusajili laini zao za simu kwa kutumia vitambulisho vinavyokulika kiserikali ili kupunguza uhalifu wa kimtandao ambao umeshamiri katika maeneo mbalimbali nchini.

Meneja Miradi ya Airtel Kanda ya Ziwa Joseph Mushi amesema kufunguliwa kwa duka hilo ni mwendelezo wa kampuni yake kusogeza huduma karibu kwa wateja badala ya kuzifuata kwenye maduka makubwa mijini.

“Duka hili la kisasa ni moja ya maduka 27 ya kanda ya ziwa,na nila 13 mkoani Mwanza litatoa huduma zote zinazopatikana kwenye maduka makubwa,na hakuna kuwa na upungufu wa kutoa fedha….alisema Mushi

Kwa upande wake Afisa mtendaji wa kata ya Nyegezi Charles Muso mbali nae aliipongeza Airtel kwa kuboresha huduma zake pamoja na kuwashauri wananchi walioko pembezoni kulitumia duka hilo kupata huduma za kimtadao.

“Ukweli duka hili sasa litawafanya wananchi waliokuwa wakitumia nauli zao kufuata huduma mjini karibu kilometa 15 sasa wamepata mkombozi..alisema Muso

Jumla ya mikoa 10 imezindua maduka ya kisasa ka ajili ya kusogeza huduma karibu kwa wateja, mikoa hiyo ni pamoja Morogoro,Pwani,Mwanza,Kagera,Kigoma,Mara Dodoma,Singida,Pwani na Dar es Salaam.

No comments: