Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Helene Weesie |
Dar es Salaam
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti (SBL) Helene
Weesie, jana alifanya mazungumzo na maofisa kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani
ikiwa ni sehemu ya uboreshaji zaidi wa maslahi na mazingira ya kazi kwa
wafanyakazi wa kampuni hiyo.
“Tukiwa kama kampuni
inayoheshimu sheria na kujali maslahi ya wafanyakazi wetu na nchi kwa ujumla,
tumekuwa tukikutana na mamlaka husika ili kuhakikisha haki na maslahi ya
wafanyakazi wetu yanalindwa na kuheshimiwa.,” anasema Weesie
SBL imeajiri wafanyakazi zaidi ya 700 katika viwanda vyake
vilivyopo Moshi, Mwanza na Dar es Salaam. Bia yake mama ya Serengeti Premium
Lager ilizalishwa kwa mara ya kwanza kwa kutumia kimea kwa aslimia 100 na
imeweza kushinda zaidi ya tuzo kumi za dhahabu za kitaifa na kimataifa.
Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2002, SBL imekuwa huku ikiongeza
idadi ya bidhaa inazozalisha. Baada ya kisisi iikubwa cha hisa kuchukuliwa na
Kampuni ya Bia ya AFRIKA Mashariki (EABL)/Diageo mwaka 2010 kumekuwepo
uwekezaji mkubwa amboa umefanikisha uzalishaji w3a bidhaa zenye ubora wa
kimataifa na kutengeza fursa kwa Watanzania.
Moja kati ya nguzo za Diageo ambayo ni kampuni mama YA sbl ni
kujenga na kuwawezesha wafanyakazi wake sehemu yoyote inapofanya kazi ikiwamo
Tanzania. Kutokana na hili idadi ya wataalamu wageni imepungua kwa kiasi
kikubwa kutoka zaidi ya 30 hadi sita kufikia mwezi Machi 2018 ikiwa ni chini ya
asilimia 1 ya nguvu kazi katika kampuni
“Tunapenda kuwahakikishia wateja wetu kuwa tutaendelea
kuimarisha mahusiano na wafanyakazi wetu. Tutaendelea kukidhi mahitaji
yao kwa kuwahakikishia bidhaa bora ikiwa ni sehemu muhimu kwa biashara
yetu,”anasema mkurugenzi huyo.
No comments:
Post a Comment