Tangazo

September 9, 2011

Hongera Michuzi Blog kwa kutimiza Miaka Sita

Mwanahabari na Mwanablogu mashuhuri, Muhidini Issa Michuzi
Ikiwa imetimia miaka sita tangia Blog ya Jamii ianze kufanya kazi, timu nzima ya Blogu ya Daily Mitikasi inaungana na wadau wote kumpongeza Ankali Michuzi, licha ya kuwa blogu yetu hii bado ni changa na ina umri wa miezi miwili tuu toka ianzishwe lakini inatambua kazi nzuri inayofanywa na Michuzi Blog katika kuitumikia jamii yake na pia naweza kusema kuwa Blogu ya Michuzi ndiyo hasa iliyonihamasisha nami kuona umuhimu wa kuwa Mwanablogu kwa msemo mwingine ndiyo iliyonifumbua macho. Ankal tunakutakia Kila La Heri.
 
Imetolewa na:
John Hans Badi
Founder & Chief Editor
Daily Mitikasi Blog

No comments: