Tangazo

September 8, 2011

KUELEKEA MIAKA 50 YA UHURU

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Sethi Kamuhanda (katikati) akitoa ufafanuzi  kwa waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo kuhusu matumizi ya Nembo ya  Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara  na Maonesho makubwa ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara yatakayofanywa na Wizara hiyo huko la Butiama, Musoma kuanzia Oktoba 7-14 Oktoba na kutoa wito kwa wananchi kujitokeza kushiriki maonesho hayo na kuitumia nembo hiyo kwenye shughuli mbalimbali zikiwemo za biashara. Kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa wizara hiyo,  Mulwa Msongo na Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Raphael Hokororo.

Msanii mkongwe wa Bendi ya Muziki wa Dansi ya Kilimanjaro (Njenje), Waziri Ally (wa pili  kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo kuhusu Tamasha la Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara litakalowajumuisha wasanii wakongwe (wazee) na wale wa kizazi kipya (Bongo Fleva) wapato 40 litakalofanyika katika ukumbi wa Diamondi Jubilee wakati wa kilele cha maadhimisho hayo Desemba 9, 2011 ambapo nyimbo mbalimbali zilizoimbwa kuanzia miaka ya 1961 – 2011 zitaimbwa kwa ushirikiano.

Msanii na kiongozi wa B. Band, Banana Zolo (kushoto) akiweka msisitizo wa ushiriki wa wasanii wa kizazi kipya na wale wakongwe katika Tamasha la pamoja la Maadhimisho ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara litakalofanyika Diomond Jubilee Desemba 9. Wengine ni Mwakilishi wa kundi la TMK Family (wa pili kushoto), Said Fella,  Mzee King Kii (katikati) na Waziri Ally.PICHA ZOTE/ARON MSIGWA WA MAELEZO

No comments: