Tangazo

October 18, 2011

Abiria 30 wanusurika Kifo katika Ajali mbaya ya Bus Mkoani Mbeya



Bus la abiria lililokuwa likifanya safari zake kati ya Mwanjelwa jijini Mbeya hadi Mji mdogo wa Mbalizi Wilaya ya Mbeya vijijini,  limepata ajali mbaya katika mteremko wa Mbalizi ambapo zaidi ya abiria 30 wamenusurika kifo, baada ya gari kushindwa kupandisha mlima hali iliyopelekea kupinduka. Tukio hili limetokea siku ya Jumapili.

Wakazi wa Jiji la Mbeya wamelitaka Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoani humo kufanya uchunguzi wa kina ili kuweza kubaini magari yenye karoso kwa lengo la kuepusha ajali zisizokuwa za lazima. Picha na Mbeya Yetu Blog

No comments: