Tangazo

October 18, 2011

Kundi la Hamas kumwachilia Huru Mwanajeshi wa Israel

Wafungwa wakisafirishwa.
Mwanajeshi mmoja wa Israel Gilad Shalit, anatarajiwa kuachiliwa huru baadaye leo, baada ya kuzuiliwa kwa miaka mitano, huku wafungwa wa Palestina wapatao 1,000 wakiachiliwa huru kufuatia makubaliano na kundi la Hamas.
Shalit mwenye umri wa miaka 25, alitekwa nyara mwaka wa 2006 na wanamgambo wa Hamas ambao walipitia njia za chini ya ardhini kuingia Israeli kutoka Gaza.

Hapo jana mahakama ya juu nchini Israel ilikataa ombi la familia za waathirika wa mashambulio yaliyotekelezwa na wanamgambo wa Palestina, kutaka ubadilishanaji huo wa wafungwa ucheleweshwe kwa saa 48.

Kundi la kwanza wa wafungwa 477 wa Palestina wataachiliwa huru mapema hii leo.

Wengine wapatoa 550 wanapangiwa kuachiliwa huru mwezi ujao.

Katika barua aliyoiandika kwa familia za waathirika, Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema, '' Naelewa ugumu mlionao kukubali kuwa maovu yaliyotekelezwa dhidi ya wapenzi wenu hayatalipwa kama inavyopaswa''.

Wakati huo huo mjini Gaza, kundi la Hamas linajiandaa kuwakaribisha wafungwa 295 wanaotarajiwa kupelekwa katika eneo hilo.

Waziri wa mambo ya ndani huko Gaza amewasihi wakazi ''kujizuia kutumia silaha na mabomu kuelezea furaha yao''.
Source: BBC Swahili.

No comments: