Tangazo

October 15, 2011

MAKAMU WA RAIS, DK. BILAL AWASHA MWENGE WA UHURU NA KUTEMBELEA KABURI LA MWL. NYERERE BUTIAMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiweka shada la mauwa kwenye Kaburi la Hayati Baba wa Taifa Mwalim Julius Nyerere baada ya misa maalum ya kumkumbuka muasisi huyo Taifa la Tanzania iliyofanyika jana kijijini kwake Mwitongo Butiama.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Mwenge wa uhuru kiongozi wa mbia za mwenge huo mwaka 2011 2012 Mtumwa Rashid Halfan kutoka mkoa wa Kaskazini Unguja, kwa ajili ya kuanza mbio za kukimbiza katika mikoa yote ua Tanzania baada ya kuuwasha rasmi jana katika kijiji cha Butiama Mkoani Mara.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muunganowa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzinduwa kanuni za sheria ya Filamu na Michezo ya kuigiza iliyoambatana na maadhimisho ya miaka 50 Uhuru wa Tanzania Bara zilizofanyika jana katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mara. Kulia Waziri wa Habari utamaduni na Michezo Mhe. Dkt Emanuel Nchimbi.

Muandishi wa Habari wa Idara ya Habari Maelezo Anna Itenda kwa niaba ya waandishi wa habari wa Tanzania akiweka shada la mauwa katika kaburi la Baba wa Taifa Hayati Mwalim Julius Nyerere wakati wa misa maalum ya kumkumbuka muasisi wa Taifa la Tanzania iliyofanyika jana kijijini kwake Mwintongo Butiama. Picha zote na Amour Nassor VPO


No comments: