Tangazo

October 13, 2011

STANDARD CHARTERED BANK YAADHIMISHA SIKU YA KUONA DUNIANI

Wafanyakazi wa Standard Chartered Bank pamoja  na wabia wake ikiwemo Asasi zisizo za Serikali wakifanya mazoezi ya viungo kabla kuanza kwa matembezi ya “Kuona ni Kuamini” yaliyoanzia katika Ofisi za Makao Makuu ya Benki hiyo International House Mtaa wa Garden jijini Dar es Salaam leo hadi viwanja  vya Mwembe Yanga ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha 'Siku ya Kuona Duniani' ambapo kulikuwa na kambi ya macho kwa ajili ya kutoa huduma za macho bure. Benki ya Standard Chartered ilikuwa na matukio ya kuchangisha fedha kwenye masoko yake 70,  ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wa kukusanya Dola za Marekani  milioni 100, kwa ajili ya kampeni yake ya 'Kuona ni Kuamini' ikishirikiana pamoja na wabia wake ikiwemo Asasi zisizo za Serikali ili kusaidia kutokomeza tatizo la upofu. PICHA ZOTE/JOHN BADI WA DAILY MITIKASI BLOG
Kikosi cha bendi cha Jeshi la Polisi kikiongoza matembezi.
Matembezi yanaanza yakiongozwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Jeremy Awori (Kulia).
Mgeni Rasmi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Bernard Makali (katikati), Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Jeremy Awori (kulia) na Mkuu wa Mahusiano wa Benki hiyo, Juanita Mramba (kushoto) wakiongoza wafanyakazi na wadau wakuu kwenye matembezi hayo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Jeremy Awori (katikati) akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kuanza kwa matembezi hayo.
Mgeni Rasmi, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Bernard Makali akisoma hotuba yake kabla ya kuanza matembezi. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Jeremy Awori na Ofisa wa CCBRT.

No comments: