Tangazo

November 17, 2011

28 WAITWA TIMU YA KILIMANJARO STARS

Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars), Charles Boniface Mkwasa (kulia) na Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura.          

                    

Kocha Mkuu wa timu ya Tanzania Bara (Kilimanjaro Stars), Charles Boniface Mkwasa ameteua wachezaji 28 kuunda kikosi hicho kwa ajili ya michuano ya Kombe la Chalenji itakayofanyika Dar es Salaam kuanzia Novemba 25 mwaka huu.

Wachezaji walioteuliwa ni Juma Kaseja (Simba), Deo Munishi (Mtibwa Sugar) na Shabani Kado (Yanga). Mabeki wa pembeni ni Shomari Kapombe (Simba), Godfrey Taita (Yanga), Juma Jabu (Simba) na Paul Ngelema (Ruvu Shooting).

Mabeki wa kati ni Juma Nyoso (Simba), Said Murad (Azam), Erasto Nyoni (Azam) na Salum Telela (Moro United). Viungo ni Shabani Nditi (Mtibwa Sugar), Ibrahim Mwaipopo (Azam), Nurdin Bakari (Yanga), Mwinyi Kazimoto (Simba), Haruna Moshi (Simba), Ramadhan Chombo (Azam), Rashid Yusuf (Coastal Union), Jimmy Shogi (JKT Ruvu Stars) na Mohamed Soud (Toto Africans).

Washambuliaji ni Mrisho Ngasa (Azam), Mbwana Samata (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Gaudence Mwaikimba (Moro United), John Bocco (Azam), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo- DRC), Hussein Javu (Mtibwa Sugar), Daniel Reuben (Coastal Union) na Nizar Khalfan (Vancouver Whitecaps, Canada).

MAPATO STARS v/s CHAD

Pambano la mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2014 nchini Brazil- raundi ya mtoano kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Chad lililochezwa Novemba 15 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam limeingiza sh. 78,389,000.

Mashabiki waliokata tiketi kushuhudia pambano hilo ni 29,111. Viti vya kijani na bluu ambavyo kiingilio kilikuwa sh. 2,000 ndivyo vilivyovutia mashabiki wengi ambapo walikuwa 23,748 ikiwa ni zaidi ya asilimia 80 ya mashabiki wote walinunua tiketi kwa ajili ya viti hivyo.

VIP A ambapo ndipo kulikokuwa na kiingilio cha juu cha sh. 20,000, jumla ya mashabiki 187 walinunua tiketi kwa ajili ya eneo hilo. VIP B ambapo kiingilio kilikuwa sh. 10,000, mashabiki walionunua tiketi walikuwa 1,181.

Viingilio vingine katika pambano hilo vilikuwa sh. 5,000 kwa VIP C ambapo waliingia mashabiki 1,678 wakati mashabiki 2,319 walikata tiketi kwa viti vya rangi ya chungwa ambapo kiingilio kilikuwa sh. 3,000.

 VIONGOZI WALIOCHAGULIWA KUONGOZA FAM

Uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Mara (FAM) ulifanyika Novemba 13 mwaka huu wilayani Rorya.

Uchaguzi huo uliendeshwa na Kamati ya Uchaguzi ya FAM chini ya Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Viongozi waliochaguliwa kwa kuzingatia Katiba ya FAM na Kanuni za Uchagzui za wanachama wa TFF ni wafuatao;

Fabian Samo amefanikiwa kutetea wadhifa wake wa Mwenyekiti huku Deogratius Rwechungura akichaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti. Wengine waliochaguliwa ni Mugisha Galibona (Katibu Mkuu), Samwel Silasi (Katibu Msaidizi), Evans Liganga (Mhazini), David Sungura (Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF), William Chibura (Mwakilishi wa Klabu) na Valerian Goroba (Mjumbe).

Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

No comments: