Tangazo

November 17, 2011

Wakati Machinga na Polisi wakipambana jijini Mbeya Mkuu wa Mkoa Kandoro alikuwa akiwatumikiaWananchi Vijijini.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya akizungumza na waandishi wa habari juu ya miradi mbalimbali ya kijamii alipotembelea vijijini wakati huo huo Jijini Mbeya vurugu ikiibuka kati ya Machinga na Jeshi la Polisi.

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro alikuwa ndani ya gari hili akivuka kutokea katika mradi mkubwa wa kilimo cha Umwagiliaji uliopo Naming'ong'o katika kijiji cha Nkala kata ya Chitete wilayani Mbozi, wakati Bw.Kandoro akiwa huku akijitoa mhanga kupita ndani ya maji marefu wamachinga Jijini Mbeya walikuwa wakipambana na askari Polisi na kusababisha vurugu kubwa,Bw. Kandoro alilazimika kukatisha ziara yake ya wilaya ,Mbozi na kurudi Jijini Mbeya kufuatia viurugu hizo. Picha na Mbeya Yetu blog

No comments: