Tangazo

November 21, 2011

WAMA WAKUTANA NA WADAU WAO JIJINI DAR

Baadhi ya Washiriki katika mkutano wa wadau kutoka sekta binafsi ya kuwashirikisha katika kuchangia mradi wa miaka mitano wa Pamoja Tuwalee unaofanywa na Taasisi ya WAMA pamoja na FHI kwa lengo la kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu nchini. Mradi huo  unafadhiliwa na na msaada kutoka  Marekani (USAID). Mradi wa Pamoja Tuwalee unaendesha shughuli zake katika ukanda wa Pwani kwenye  Wilaya 25,  ziliopo katika Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro na Zanzibar.

Katibu Mtendaji wa Taasisi ya WAMA nchini, Daudi Nasibu akichangia katika mkutano wa siku moja wa wadau kutoka sekta binafsi ya kuwashirikisha katika kuchangia mradi wa Pamoja Tuwalee unaofanywa na WAMA pamoja na FHI kwa lengo la kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu, uliofanyika katika viwanja vya WAMA jijini Dar es Salaam Novemba 18.2011. (Picha na Mwanakombo  Jumaa-MAELEZO)

No comments: