Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye akikimbiza Bendera ya Taifa baada ya kuingia katika lango kuu la kuingilia katika Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro Marangu Mkoani Kilimanjaro jana kabla ya kuwakabidhi vijana watatu Daniel Ngowi (kushoto), Aloice Joseph (wa pili kushoto) na Raymond Ngowi (wa pili kulia) ambao wataipandisha juu ya Mlima wa Kilimanjaro kukamilisha Mbio za Bendera ya Taifa za Kili kupitia Kampeni ya Jivunie utanzania inayoenda sambamba na miaka 50 ya Uhuru kwa udhamini wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager. Wa tatu kushoto ni Meneja wa Bia ya Kilimanjaro, George Kavishe na wa pili Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Moshi, Alhaj Mussa Nsamizi. |
2 comments:
kaka mwili huo,fanya mazoezi punguza gambe
Kaka naona kazi zinaendelea vizuri. Sasa vikao vyetu vipi tena, hata moja moja tu zinatosha.
Post a Comment