Tangazo

December 7, 2011

Ewura yaipa kibali cha kuzalisha Umeme wa Upepo nchini kampuni ya Wind EA

Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu  (kulia), akimkabidhi leseni ya uzalishaji wa umeme wa upepo,  Rashid Shamte ambaye ni Mkurugenzi wa kampuni ya Wind EA, katika hafla fupi iliyofanyika jijini Dar esSalaam Desemba 07.2011. Kampuni hiyo imepewa leseni ya kuzalisha umeme wa upepo wa 100mw kwa kipindi cha Miezi 30.
                                           ********************************************
Na Mwandishi wetu

MAMLAKA YA Udhibiti wa Nishati ya Maji (Ewura) imeipatia leseni ya uzalishaji wa umeme wa upepo kampuni ya Wind East Africa ili kuzalisha umeme huo hapa nchini.

Akizungumza katika makabidhiao hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Rweura, Bw. Haruna Masebo alisema kuwa hatua ya kuidhinisha kampuni ya Wind EA kusimamia na kuteleza mradi huo imetokana na kuridhika na utendaji wake na kukidhi vigezo.

Bw. Masebo alisema kuwa kampuni hiyo imeweza kufuata masharti yote yaliyowekwa na kuwa kampuni ya kwanza nchini kuingia katika biashara ya uzalishaji wa umeme.

“Ni faraja kubwa kuona kuwa Kampuni inayomilikiwa na wadhawa kuingia katika biashara hii, tumeridhika na mipango yao hasa baada ya kukamilisha masharti yote yaliyowekwa pamoja na huifadhi wa mazingira,” alisema Bw. Masebu.

Alisema kuwa kibali hicho ni cha miezo 30 na wanatarajia kuona matunda mazuri ya kuondoa tatizo la nishati ya umeme nchini.

Mkurugenzi wa Wind EA, Bw. Rashid Shamte alisema kuwa wanafuraha kupata kibali hicho na watanzania watarajie kuwa tatizo hilo litaisha mara baada ya kukamilika kwa mradi huo.

Bw. Shamte alisema kuwa pamoja na kupewa miezo 30, wanatarajia kukamilisha mradi huo mradi huo mapema iwezekanavyo mara baada ya kukamilisha mikakati yao ikiwa pamoja na mkopo kutoka benki ya dunia.

Alisema kuwa wamezingatia masharti yote yaliyowekwa ikiwa pamoja na kutoathiri mazingira ya eneo la mradi huo tofauti na miradi mingine.

“Tumekuwa makini sana na hilo kwani tuna watalaam wa hali ya juu, tunashirikiana na wadau mbali mbali ili kufanikisha uzalishaji wa 100mw kwa watanzania,” alisema Bw. Shamte.

Aliongeza kuwa walifanya utafiti wa mradi huo mwaka jana mwezi Novemba na wizara husika iliwajibu kuridhishwa na maendeleo na mikakati yao mwaka huu mwezi wa pili.


No comments: