Tangazo

December 7, 2011

MIAKA 50 YA UHURU: VILABU VYA JOGGING VYA KINONDONI VYAFANYA HARAMBEE YA KUCHANGISHA FEDHA KWA AJILI YA KUFANIKISHA SHUGHULI YA KUFANYA USAFI NA KUTOA MISAADA KWA WAGONJWA KATIKA HOSPITALI YA MWANANYAMALA.

Siku ya Jumapili, tarehe 4 Disemba, 2011 katika hafla ya uzinduzi wa Royal Billy's Lodge ambayo ipo nyuma ya Kanisa KKKT Tangi-Bovu palifanyika pia harambee kwa ajili ya kuchangia shughuli ya kufanya usafi wa mazingira katika Hospitali ya Mwananyamala pamoja na kutoa misaada ya hali na mali kwa wagonjwa katika wodi ya wazazi na wodi ya watoto hospitalini hapo. Kabla ya kuanza kwa hafla ya uzinduzi wa lodge hiyo na harambee, wakimbiaji wa mbio za pole pole (jogging) kutoka vilabu vya Biafra, Namanga, Kunduchi, Mbezi Beach, Temeke na wenyeji Tangi Bovu walikimbia mbio hizo kutoka Tangi Bovu kupitia Kawe na kurudi Tangi Bovu. Pichani baada ya mbio za pole pole kumalizika wakimbiaji waliendelea kufanya mazoezi kwa mtindo wa aerobics na kama kawaida ili aerobics inoge basi unapigwa muziki na kaka Michael J almaarufu Mopao anaongoza mazoezi hayo.

Mmoja wa Wakurugenzi wa Royal Billy's Lodge ndugu Tobias Owur akiingia wa mwisho baada mbio za pole pole - wakimbiaji wengi hawakumaliza mbio kwa kukimbi kama zilivyoanza.

Kutoka Kushoto ni Mama Kenisha Mkurugenzi wa Biafra Sports Club, Tobias Owur mmoja wa wakrugenzi wa Royal Billy's Lodge na Abdul A. Mollel Mwenyekiti wa Biafra Sports Club.

Wana-jogging wengine waliona viatu ni vizito na havivaliki tena.

 Dada Edita wa Namanga Jogging akinyoosha kiuno baada ya mbio.

 Wakiwakilisha Biafra - Kutoka kushoto Jacqueline Mugalura, Yahya Poli na Ally Masharubu.

 Mbusilo Joseph - katibu wa Kunduchi Kwanza pamoja na KP wa Temeke Jogging.

Baada ya kumaliza mbio na burudani za hapa na pale, wana-jogging waliingia ukumbini kwa ajili ya kuanza harambee. Ndugu David Mwaka ambaye ni Mwenyekiti wa Namaga Jogging na Mkurugenzi wa Esoshi General Trading akiwakaribisha wageni ukumbini.

Katibu wa Kamati ya maandalizi akiweka mambo ya teknolojia sawa sawa akiwa sambamba a mhamasishaji wa kamati toka klabu ya namanga Charles Juma.

Mdau Henry Byarugaba akiingia ukumbini, yeye pamoja na mchango wa fedha ameongeza pakiti 100 za maziwa ya Tanga Fresh toka kwenye idadi ya awali ambayo 400 hivyo kufikisha idadi ya pakiti 500.

Mhamasishaji wa kamati Charles Juma alipigishwa magoti na kugombolewa ambapo pesa iliyopatikana iliongezewa kwenye mahitaji ya kukamilisha shughuli hiyo.

 Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi Abdul Mollel akihesabu sehemu ya fedha zilizokusanywa papo hapo kwenye harambee.

Meza iliwakilishwa na Mollel (kushoto), ndugu Joseph Mwaka (katikati) na Mjomba Ole.

No comments: