Mwenyekiti wa Taasisi ya Hassan Maajar Trust (HMT), Balozi Mwanaidi Sinare Maajar. |
Mwenyekiti wa Taasisi ya Hassan Maajar Trust (HMT) Balozi Mwanaidi Sinare Maajar na Mwenye Kiti wa Bank M, Mheshimiwa Nimrod Elirehema Mkono wameandaa hafla ya chakula cha jioni ili kuchangisha fedha kwa ajili kuboresha mazingira ya kusoma nchini kote.
Hafla hiyo ya chakula cha jioni kwa ajili ya kuondoa uhaba wa madawati na viti mashuleni inajulikana kama “Dawati kwa Kila Mtoto”

Akizungumza katika hafla hiyo juzi, Balozi Mwanaidi Maajar alisema “Wakati wa uzinduzi wa taasisi ya Hassan Maajar Trust mwezi Julai mwaka huu, tuliahidi kuwa ndani ya kipindi cha miezi sita tangu kuzinduliwa, tungeanza kampeni kubwa yenye lengo la kukusanya shilingi bilioni 3 katika kipindi cha miaka 2 hadi 3 kwa ajili ya ununuzi wa madawati na viti kwa shule za msingi ili kuboresha mazingira ya kusoma kote nchini”
Leo hii tunajumuika pamoja kwenye hafla hii ya chakula cha jioni,tukitimiza azma yetu ya kuondoa tatizo la madawati mashuleni, leo hii tunaposherekea miaka 50 ya uhuru nawasihi wageni wote waalikwa na wadau wa maendeleo na tutambue kua, idadi ya madawati na viti nchini bado ni mbaya sana kwenye taifa letu, watoto wetu wanahitaji mazingira bora ili kupata elimu bora, na hili ni jukumu la kila mmoja wetu kwenye hafla hii kuona umuhimu wa yeye kuchangia ili kupiga vita dhiti ya mazingira mabovu ya elimu. alisema Balozi Mwanaidi
Madhumuni ya hafla hii ni kuhamasisha jamii kuona umuhimu wa kuchangia na kuweka mazingira ya shule zetu kuwa mahali muafaka kwa watoto wetu kusoma na kujiendeleza
Sisi sote tumeshuhudia jinsi watoto wanavyoteseka kutokana na kukosa viti na madawati mashuleni, elimu bora haiji bila mazingira bora ya kusoma.
Sisi Bank M kwa ushirikiano wa Taasisi ya HMT, kama sehemu yetu ya kusaidia jamii yaani “Corporate Social Responsibility” tumetambua umuhimu wa kafadhili hafla hii kwa ajili ya kuchangia madawati na kuboresha mazingira ya elimu ili kuhakikisha kuwa watoto wetu wanapata madawati na vifaa vingine muhimu wawapo shuleni.
Kampeni ya Dawati kwa Kila Mtoto ni kampeni muhimu sana ambayo Bank M imefurahi kushiriki”.Alisema Mwenye Kiti wa Bank M Mheshimiwa Nimrod Elirehema Mkono

Nae Mwenyekiti wa HMT, Balozi Mwanaidi Maajar, aliongezea kwa kusema, "Kampeni itaendeshwa kwa jina la Dawati kwa kila Mtoto au A Desk for every child kwa kiingereza, na itafanyika nchini Tanzania na Marekani.
Kwa mujibu wa takwimu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi zinaonyesha kuwa shule za msingi zina uhaba wa takriban madawati na viti milioni 3.Hivyo basi tunatoa wito wa wadau wote tufanye juhudi zote ili kutatua tatizo hili
Kuna uwezekano mkubwa wa kumwezesha kila mtoto nchini kupata dawati na kiti katika kipindi cha miaka miwili hadi mitatu ijayo, lakini suala hili linahitaji mshikamano kwa kila mtu kutoka nyanja tofauti na jamii nzima kwa ujumla kuona umuhimu wa kusaidia kufanikisha jambo hili.
Pamoja na hafla hii, tutatumia njia mbalimbali kukusanya michango, ikiwa ni pamoja na maombi ya moja kwa moja kutoka kwa wananchi kupitia simu za mkononi na pia kuomba makampuni zingine na wafadhili wa ndani na nje ya nchi kuelekeza nguvu zao katika upatikanaji wa madawati yaliyo bora na yenye kudumu.
Tatizo la uhaba wa madawati ni aibu kwa taifa na kwa watoto, wototo wetu wanakaa sakafuni, au kukalia mawe, matofali na vitu vya aina hiyo huku sisi wazazi tukiwa tumefumbia macho suala hilo na kuona ni suala la serikali, tukijumuisha nguvu zetu kwa ushirikiano na serikali tatizo hili lazima litapungua kwa kiasi kikubwa ndani ya kipindi cha mda mfupi.alimalizia Mama Balozi.
Wakati wa hafla hiyo kiasi cha shilizi za kitanzania millioni 109,908,000 zilichangishwa na pia zilipatikana dola 1,820 za kimarekani, 20 Euros na Swiss Francs 50.

Pia ahadi zilikua million 279,058,00 na dola 21, 820 ambazo zinategemewa kukusanywa.
No comments:
Post a Comment