Tangazo

January 4, 2012

DK. JAMES MSEKELA BALOZI MPYA WA TANZANIA NCHINI ITALY

Dk. James Alex Msekela
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewateua mabalozi wawili kuanzia Oktoba 12, mwaka jana, 2011, Katibu Mkuu Kiongozi, Bwana Ombeni Yohana Sefue ametangaza jana, Jumanne, Januari 3, 2012.

Katika taarifa yake, Katibu Mkuu Kiongozi Sefue amesema kuwa Rais Kikwete amemteua Dkt. James Alex Msekela kuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia. Kabla ya hapo Mheshimiwa Msekela alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

Aidha, taarifa hiyo ya Bwana Sefue imesema kuwa Rais Kikwete amemteua Bwana Ramadhani Muombwa Mwinyi kuwa Naibu Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, New York. Kabla ya hapo, Bwana Mwinyi alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Katibu Mkuu Kiongozi amesema katika taarifa yake kuwa wateuliwa hao wawili wataapishwa kesho, Alhamisi, Januari 5, 2012.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

No comments: