Tangazo

January 4, 2012

MWILI WA BALOZI MHINA WAAGWA DAR, KUZIKWA LEO KOROGWE TANGA

Makamu wa Rais, Dk. Moahammed Gahrib Bilal akiongoza sala maalum ya kuombea marehemu mbele ya jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi ya CCM, Balozi Athumani Mhina, kabla ya mwili huo kusafirishwa jana  kwenda Korogwe kwa mazishi. Shughuli hiyo ilifanyika nyumbani kwa marehemu, Wazo, Dar es Salaam.PICHA ZOTE/BASHIR NKOROMO

Vijana wakibeba jeneza lenye mwili wa Balozi Mhina ulipowasili nyumbani kwa marehemu, Wazo ukitolewa hospitali ya Lugalo.
 

Masheikh na Wanazuoni wakisoma kisomo maalum cha kmuombea marehemu Balozi Athumani Mhina.
 

Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa akitia saini kitabu cha maombolezo, nyumbani kwa marehemu Balozi Mhinam Wazo, Dar es Salaam, kabla ya shughuli ya kusafirisha mwili kwenda Korogwe Tanga.
 

Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama akitia saini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Balozi Mhina, Wazo kabla ya kusafirisha mwili kwenda Korogwe, Tanga jana.
 

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akisaini kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Balozi Mhina, kabla ya mwili kusafirishwa kwenda Korogwe jana.
 

Wanafamilia wakiwa katika majonzi wakati wa shughuli ya kusaifirishwa mwili wa marehemu.
 

Makamu Mkt wa CCM (Bara) Pius Msekwa, Mukama na Nape wakizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Omari Chambo wakati wa shughuli ya kuaga mwili wa marehemu Balozi Mhina, Wazo, Dar es Salaam jana.

Katibu Mkuu wa CCM, Mukama akimfariji, Makamu Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi (Zanzibar) Dogo Mabrouk wakati wa shughuli za kusafirisha mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Jumuia hiyio Balozi Mhina.

Wasira akijadili jambo na Nape kwenye shughuli hiyo ya kusafirisha mwili wa marehemu Balozi Mhina leo. Kulia ni Katibu wa NEC, Uchumi na Fedha CCM, Mwigulu Nchemba.
 

Makamu wa Rais, Dk. Bilal akimpa pole Makamu Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi Dogo Mabrouk.
 

Waziri Nchimbi akifarijiana na Naibu waziri wa Nishati na Madini Adamu Malima (kulia) na Mbunge wa Namtumbo, Vita Kawawa (katikati) kwenye msiba huo.
 

Katibu wa Jumuia ya Wazazi Kinondoni, Stanley Mkandawile akijadiliana jambo na Mwenyekiti wa Jumuia hiyo Tabora, Aden Rage, Mwenyekiti wa Wazazi  Mkoa wa Dar es Salaam, Azzan Zungu na Waziri wa zamani, Iddi Simba, kwenye msiba huo.

No comments: