Tangazo

February 6, 2012

JK ATUA JIJINI MWANZA, KUWA MGENI RASMI MIAKA 35 YA CCM

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimbusu mtoto Nyambani Mganga (3) baada ya kuviwa na uchezaji ngoma wake, katika kikundi cha  Utandawazi Theatre cha Ukerewe, kilipokuwa kikitumbuza kabla kabla ya Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwanza kwa ajili ya maadhimhso ya miaka 35 ya CCM.

Mwenykiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete akimtuza mtoto Nyambani Mganga (3) baada ya kuvutiwa na uchezaji ngoma wake, katika kikundi cha Utandawazi Theatre cha Ukerewe, kilipokuwa kikitumbuza alipowasilleo kwenye Uwanja wa Ndege wa Mwanza kwa ajili ya kuwa mgeni rasmi kwenye sherehe za miaka 35 ya CCM zitakazofanyika jijini Mwanza.
 

Jk akishuka kwenye ndege alipowasili uwanja wa Ndege wa Mwanza.

Rais Kikwete akisalimiana na mkuu wa mkoa wa Mwanza  Injinia Evarist Ndikillo baada ya kuwasili Uwanja wa ndege jijini Mwanza.

Rais Kikwete akifuatana na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza  Mabina wakati alipowaisli jijini Mwanza.

Rais Kikwete akiwasalimia wanachama wa CCM baada ya kuwasili jijini Mwanza.

Katibu wa NEC, Nape Nnauye, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Mabina na Katibu wa CCM  Mukama wakisahuriana jambo kwenye Uwanja wa Ndege jijini mwanza wakati wa mapokezi ya Rais Kikwete (Picha zote na Bashir Nkoromo)

No comments: