Tangazo

February 6, 2012

RAIS KIKWETE AONGOZA MATEMBEZI MIAKA 35 YA CCM

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasili kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Mwanza kuongoza matembezi ya mshikamano kwa ajili ya maadhimnisho ya miaka 35 ya CCM jana. Anayempokea ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa na wengine ni Spika wa Bunge Anna Makinda ambaye ni mlezi wa mkoa huo na Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama. Pamoja na  Rais Kikwete ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Clement Mabina na Mkuu wa mkoa wa Mwanza  Evarist Ndikilllo. (Picha zote na Bashir Nkoromo)

Kikwete akimsalimia Katibu Mkuu wa CCM mstaafu, Philip Mangula kabla yamatembezi kuanza Ofisi ya CCM mkoa wa Mwanza. Kulia ni Katibu Mkuu Mstaafu Yussuf Makamba.
 

Rais Kikwete akimsalimia Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kabla ya matembezi hayo.
 

Wananchi kutroka maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mwanza wakiwa kwenye Ofisi ya CCM mkoa huo tayari kushiriki matembezi hayo.

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, Mama Salma Kikwete wakiongoza matembezi hayo kutoka kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Mwanza hadi viwanja vya Furahisha jijini Mwanza akiwa na viongozi wa ngazi ya juu wa CCM. Kutoka Ofisi hiyo hadi kwenye viwanja ni umbali wa kilometa tatu.

Katibu Mkuu wa CCM Wilson Mukama akiwa na Makatibu wastaafu wa CCM, Yussuf Makamba na Philip Mangula kabla yamatembezi kuanza.
 

Vijana wa Sungusungu wakijifua kabla ya matembezi kuanza.
 

Kijana Mussa aliyemwagiwa tindikali wakati wa kampeni za ucxhaguzi mdogo jimbo la Igunga mwaka jana, akishiriki matembezi hayo. Wapili kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.
 
Wananchi wakiushangilia msafara wa matembezi hayo ulipopita eneo la mtaa wao.
 

Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kiwkete akiwasalimu wananchi baada ya kufika mwisho wa matembezi hayo kwenye Viwanja vya Furahisha jijini Mwanza.
 

Matembezi yakiingia kwenye Viwanja vya Furahisha.
 

Sungusungu wakionyesha ukakamavu wao baada ya Kikwete kuwasili nba matembezi hayo kwenye viwanja vya Furahisha.

No comments: