Tangazo

February 7, 2012

OKOA MAISHA YA MAMA HUYU


Titi likiwa limeharibika kwa tatizo la kansa
Mkazi wa Frelimo katika manispaa ya Iringa Esther Maginga (60) ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa kansa ya titi toka mwaka 1996 anawaomba wasamaria wema popote nchini na duniani kujitokeza kumsaidia kuokoa maisha yake kutokana na tatizo la kansa ya titi linalomsumbuka .

Mwanamke huyo mwenye familia ya watoto sita amesema kuwa baba wa watoto hao hao uwezo wa kifedha kutokana na shughuli yake ya gereji ambayo anaifanya kutomsaidia kupata fedha ya kutosha zaidi ya kuishia kupata fedha za kodi ya nyumba na mahitaji ya nyumbani.

Hivyo alisema hata watoto wake wamekuwa wakiishi kwa msaada wa wasamaria wema ambao wamekuwa wakisaidia kusomesha watoto hao elimu ya sekondari.

Alisema ili kufanikisha kwenda Hospitali ya taifa ama KCMC kwa ajili ya matibabu ni kiasi cha shilingi milioni 2.5 zinahitajika na kwa upande wake hao hati shilingi kwa ajili ya kwenda kutibiwa hivyo kuomba wasamaria wema kuweza kumsaidia ili kunjusuru maisha yake kutokana na sasa hali ya uvimbe katika titi kuanza kuongezeka zaidi.

Kwa wale watakao guswa kuungana na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kwa ajili ya kusaidia kuokoa maisha ya mtanzania mwenzetu huyo waweza kutumia huduma ya M-PESA kwa namba 0754 026 299 ama tigo Pesa kwa namba 0712 750199 na Mungu atakubaliki kwa mchango wako.
 
 Picha na Habari kwa hisani ya Francis Godwin, Iringa

No comments: