Tangazo

March 9, 2012

Mkutano wa Rais, Dk. Kikwete na Wazee wa Dar es Salaam waahirishwa hadi Kesho Jumamosi Saa 5 Asubuhi - Diamond Jubilee Hall

Mkutano wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete na wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam uliopangwa kufanyika leo, Ijumaa, Machi 9, 2012, umeahirishwa hadi kesho, Jumamosi, Machi 10, 2012.

Mkutano huo umeahirishwa ili kutoa nafasi kwa Mheshimiwa Rais kufanya mashauriano zaidi na wadau mbali mbali kuhusu suala ambalo Mheshimiwa Rais atalizungumzia kwenye mkutano huo.

Kama ulivyokuwa mkutano ulioahirishwa leo, mkutano wa kesho utafanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee kuanzia saa tano asubuhi.

Imetolewa na Ikulu Mawasiliano
09/03/2012

No comments: