Tangazo

March 6, 2012

MSONDO NGOMA KUENDELEA KUMTAMBULISHA SHABANI LENDI WIKI HII


BENDI kongwe ya muziki wa dansi ya Msondo Ngoma inatarajia kutoa burudani  katika Jiji la  Dar es Salaam kwa ajili ya kumtambulisha mwana muziki wao mpya Shabani Lendi.

Akizungumza na Daily Mitikasi Blog, msemaji wa bendi hiyo Rajabu Mhamila 'Super D' alisema, baada ya kumtambulisha huko Zanzibar sasa wamepanga kumtambulisha siku ya Alhamisi ambapo watakuwa Kilimani Pub - Stakishari, Ijumaa Leaders Club - Kinondoni, Jumamosi TCC Klabu na Jumapili watakuwa katika ukumbi wa Max Bar Ilala Bungoni kwa ajili ya kumtambulisha kikamilifu msanii huyo.

Super D amewataka wakazi wa Dar es Salaam na Mikoa ya Jirani kuhudhuria kushuhudia burudani kali watakayoitoa ikiwa ni pamoja kusikia nyimbo zao mpya ambazo ni miongoni mwa nyimbo zitakazo kuwa katika albamu yao mpya ya mwaka huu ikiwa ni pamoja kusikiliza nyimbo zao za zamani.

Alizitaja nyimbo hizo mpya kuwa ni Suluu ya Shabani Dede, Nadhiri ya Mapenzi ya Juma Katundu, Mjomba, Dawa ya deni kulipa na lipi jema ambapo albamu hiyo inatarajia kuwa tayari hivi karibuni.

No comments: