Tangazo

March 7, 2012

NHIF YAWEKA KAMBI YA UPIMAJI AFYA STENDI KUU MKOANI SINGIDA NA KUTOA MSAADA KTK HOSPITALI ZA MKOA HUO.

DR. KUBONYA WA NHIF AKIMPA USHAURI WA NAMANA YA KULINDA AFYA YAKE KUTOKANA NA UZITO ULIOONGEZEKA BWN ALLY JUMANNE AKIWA NI MMOJA WA WAKAAZI WALIOJITOKEZA KUPIMA NA KUJUA HALI ZA AFYA ZAO  LEO MKOANI SINGIDA,NHIF IMEWEKA KAMBI HIYO MAHUSUSI IKIWA NI KUWAHAMASISHA WANANCHI KUWA NA UTAMADUNI WA KUPIMA AFYA MARA KWA MARA.

PICHANI NI BWN. DEUS KUNUWA AKIMPIMA UWIANO WA  UREFU NA UZITO WA MWILI  KITAALAMU (BMI) BWN. JOSEPH SANGAU,UHAMASISHAJI WA UPIMAJI WA AFYA KWA WANANCHI WA SINGIDA UNAKWENDA SANJARI NA SIKU YA WADAU  INAYOFANYIKA MKOANI HUMU AMBAPO  WANANCHI WANAIMIZWA KUJIUNGA NA MIFUKO YA AFYA YA JAMII KWANI NDIYO  MKOMBOZI WA HUDUMA ZA AFYA KWENYE HALMASHAURI ZAO HUSUSANI  VIJIJINI.

MJUMBE WA BODI YA WAKURUGENZI WA MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA BWN. ALEX P. MAGESA AKITOA ZAWADI YA MASHUKA 700 KWA NIABA YA HOSPITALI,ZAHANATI NA VITUO VYA AFYA MKOANI SINGIDA KWA MUUGUZI MKUU WA MKOA HUO BI.ELLETRUDE MAKOWI.

MGANGA MKUU MFAWIDHI WA HOPSITALI YA MKOA WA SINGIDA DKT. SULEMANI MTTANI (KULIA), AKIMWELEZA MJUMBE WA BODI YA NHIF BWN ALEX MAGESE MAANDALIZI YA AWALI YA UKARABATI WA JENGO(ALIPO PICHANI)  LITAKALOTUMIKA KUWAHUDUMIA WANACHAMA WA NHIF NA CHF HIVI KARIBUNI.

No comments: