Tangazo

March 12, 2012

TASAF YATUMIA BILION 5/- KATIKA MIRADI MBALIMBALI KISIWANI PEMBA

WAZIRI wa Nchi Ofisi  ya Makamo wa Rais Muungano Samia Suluhu Hasani apita Maelezo juu ya ufugaji wa Nyuki kutoka kwa katibu wa kikundi cha ushika cha kibokoni bw  khamis suleiman alipotembelea kikundi hicho kinachofadhiliwa na mfuko wa maedeleo ya jamii Tasaf pemba, wakatikati ni Mkuu wa walaya chake chake Mwanajuma Majid .

Waziri Wa Nchi Ofisi Makamo  ya Rais Mungano Samia Suluhu Hasani  akipata maelezo kutoka kwa Bw Daudi ismail  mkazi wa Wawi juu ya Bwawa la Umwagiliaji Maji katika Mashamba ya Dobi Wawi alipofika kutembelea mradi huo ambao unafadhiliwa na mfuko wa  Maendeleo ya Jamii Tasaf alipofika kukagua Ujenzi huo.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Muungano akipata Maelezo kutoka kwa Bw Khamis Feiz wakati akitembelea Ujenzi wa Barabara ya Ndugunkitu Mkoroshoni inayofadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tasaf.(Picha na  Ali Meja )
*****************
Na  Ali Meja - OMR
Mfuko wa maendeleo  ya jamii TASAF umetumia jumla ya shilling bilioni 5/- kisiwani pemba tokea mwaka 2006 katika miradi mbali mbali ya maendeleo.

Hayo yamebainishwa na maratibu wa mfuko wa TASAF pemba bwana ISA JUMA  ALI  alipokuwa akitoa  maelezowa waziri wa nchi ofisi ya makamo  wa  rais muungano mh Samia Suluhu hasani  katika ziara maalumu kisiwani pemba katika kukagua miradi mbambali ya maendeleo.

Waziri Samia yupo kisiwani pemba kwa zira ya siku tano    kujioneshughuli mbali mbali za maendeleo ktika maeneo  mbali mbali.

Akitoa mchanaganuoa wa matumizi ya miradi ya TASAF unaofadhili wa na serikali ya jamuhuri ya muungano , amesema kuwa katika maradi huo awamu ya pili wamefanikiwa zaidi ya miradi 347 imepataufadhili wa jumla ya shilling 5,544,696,611.

Miongoni mwa miradi ambayo imetembewa jana ni pamoja na mradi wa ufugaji nyuki kibokoni  ambao umefadhiliwa jumla ya shilling million kumi hadi sasa .

Pia takatika zira hiyo mradi wa umwagiliaji maji wa DOBI WAWI ambao umepatiwa ufadhili wa jumla ya milon 39,947,710, ambao utwanufaisha jumla ya wananchi elfu mbili utakapo malizika .

Katika ziara hiyo  mradi wa ujenzi wa barabara  ya machomane ndugunkitu kupitia mkoroshoni mbao naopia umejegwa kwa hisani ya mfukowa maendeleo ya jamii wametakiwa kuwa makini na utunza wa miradi huyo ambao kipindi hiki cha mvua huwa ni matatizo makubwa hasa kwa mkukos misimamizi na kusababisha haribika haraka .

Wakati wa machana mh waziri wa nchi ofisi ya rais muungano alitmbelea katika soko la samaki liliopo wesha katika wilaya ya chake chake na kuwataka walengwa wa mradi huo kudhamini vizuri sana .

Nae kwa upande wake sheha wa shehia hiyo amemwahidi mh Samia kuwa hii ndio nafsi pekee kwao kujikomboa hivyo watalitunza soko hilo kama mboni ya jicho lao .

Aidha waziri huyo wa muungano yupo kiswani pemba kwa ziara za siku tano katika mikoa miwili pemba ambapo atatembelea miradi mbali mbali katika kuhakikisha miradi inayofadhiliwa na serikali inatoa faida kubwa sana kwa maslahi ya wananchi kwa umjumla .

No comments: