Tangazo

April 18, 2012

FFU wa Ngoma Africa Band wameachia Song Jipya la "Uhuru wa Habari"

Ras Makunja

Sololist- Christian Bakotessa aka Chris-B
Kwa kawaida wanahabari na vyombo vyao ndio wanarusha hewani habari za matukio mbali mbali pamoja wasanii na burudani zao kwa jamii, lakini bendi maarufu Ngoma Africa aka FFU imewageuzia kibao !! na kuliweka hewani song jipya "Uhuru wa Habari" wimbo huo mpya utunzi wake kamanda Ras Makunja akiimba kwa kushirikiana na kijana Christian Bakotessa aka Chris-B,ambaye pia ni mpiga gitaa la solo(mtutu) wa kikosi kazi iko.

Bendi hiyo maarufu Ngoma Africa yenye makao yake kule Ujerumani, miezi michache tu iliachia hewani CD ya "Miaka 50 ya Uhuru" na sasa wanarusha hewani "Uhuru wa Habari".

Taarifa za kuaminika zinaeleza kuwa Remix ya wimbo huo pia itakua hewani siku za usoni, katika Remix hiyo kutakua na majina mengi ya wadau wa habari ambao wanachangia kuijulisha jamii habari mbali mbali.

Sikiliza na pata burudani ya bure katika ffu camp at www.ngoma-africa.com au http://www.ngoma-africa.com

No comments: