Afisa
Mtendaji Mkuu wa Shear illusions, Shekha Nasser (katikati), akizungumza na
waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kuhusu uzinduzi wa vipodozi
vyake vipya aina ya LuvTouch Manjano unatakaofanyika Mei 31 mwaka huu katika
ukumbi wa Diamond Jubilee VIP jijini. Kushoto ni Ofisa wa Programu wa Manjano
Foundation, Gugu Ndlovu na Mshauri Kiongozi wa Manjano Foundation, Sadaka
Gandhi.PICHA/JOHN BADI WA DAILY MITIKASI BLOG
xxxxxxxxxxxxxxxxxxx
DAR ES SALAAM
Shear Illusions inasherehekea mwongo mmoja wa urembo nchini Tanzania kwa kuzindua vipodozi vyake ijulikanayo kama LuvTouch Manjano!
Shear Illusions inasherehekea mwongo mmoja wa urembo nchini Tanzania kwa kuzindua vipodozi vyake ijulikanayo kama LuvTouch Manjano!
Uzinduzi
huu utafanyika tarehe 31 Mei 2015 kuanzia saa 6 mchana kwenye Ukumbi wa Diamond
Jubilee VIP Hall. Shamrashamra hizi pia itatoa fursa kwa kuendeleza mtandao wa
kibiashara kwa kina mama na pia mada mbali mbali ya jinsi ya kujikwamua
kimaisha itatolewa. Bila ya kusahau mafunzo ya jinsi ya kutumia vipodozi.
Mgeni
rasmi anatarajiwa kuwa mke wa Waziri Mkuu, Mama Tunu Pinda na mtoa mada mkuu
atakuwa ni Balozi Mwanaidi Majaar.
‘Nina
amini kwa kupendeza. Napendelea kulipuka kwenye kila mtoko. Sitegemei vinasaba
vyangu. Naamini muonekano mzuri ni kujitolea kwako na kwa wengine pia’
Mwanamitindo toka Somalia, Iman.
Shear
Illusions, imeweza kutambulisha urembo na muonekano wa mwanamke wa kitanzania
kwa Zaidi ya miaka kumi. Tumetanabaisha urembo kuanzia kujipodoa, nywele,
vipodozi na vito hadi blog na jarida inayoelezea masuala ya urembo. Baada ya
kuuza bidhaa mbali mbali ya urembo toka nchi mbali mbali, Shear Illusions inazindua rasmi bidhaa yake ya
LuvTouch Manjano.
LuvTouch
Manjano ni maalum kwa ajili ya kumpendezesha mwanamke wa kitanzania. Kuna aina
kumi ya vipodozi msingi kuanzia Mwanzi na Mpodo hadi kahawa na ardhi. Bidhaa
hizi zimezingatia hali ya hewa ya joto. Vipodozi hivi vinalengo la kuongeza
muonekano wako kwa hali yoyote.
SAFARI
YA SHEAR ILLUSIONS
2005:
Duka la kwanza la Shear Illusions ilifunguliwa jengo la Millenium Towers na
ilikuwa ni duka la aina yake nchini Tanzania kwa kuuza vipodozi na vifaa vya
nywele.
2006:
Maduka ya Shear Illusions ilifunguliwa Arusha na Mlimani City
2009:
Shear Illusions ilizindua jarida la ‘Shear Hair and Beauty’ inayomlenga
mwanamke wa kisasa wa kitanzania.
2013:
Duka la Shear Illusions lafunguliwa kwenye jingo la Kibo Commercial Complex,
Tegeta
2015:
Uzinduzi wa vipodozi aina ya LuvTouch Manjano inayomlenga mwanamke wa
kitanzania.
2015:
Shear Illusions yazindua taasisi ya ‘Manjano Foundation’ ambayo inajihusisha na
kuendeleza program maalum ya kuwawezesha jamii mbali mbali nchi nzima.
Tungependa
kushukuru kampuni zifuatazo waliojitokeza kusaidia hafla hii ya kuwawezesha
wanawake; NSSF, TCRA, Clouds Media, Maxcom, A1 Outdoor, Mr. Price, Cassandra
Lingerie, Amina Design, Maznat Bridal, Advertising Dar, Beauty Point, Hugo
Domingo, I-View Media, FAIDIKA, Benchmark Productions, Fasta Fasta, TENSHI,
Jardin Modeling Agency na mashirika mbali mbali hapa Dar es Salaam.
Kwa
taarifa Zaidi kuhusu tukio hili, tembelea tovuti ya www.manjanofoundation.org
na pia kwenye instagram na facebbok.
Kwa
kupata tiketi na maelezo mengine unaweza kuwasiliana kupitia barua pepe info@shearillusions-africa.com
au info@manjanofoundation.org
au simu ya Flora +255 772 999 603.
Asante
Shekha
Nasser
KUHUSU
SHEAR ILLUSIONS
Shear
Illusions ni duka la kitanzania linalouzabidhaa za urembo kwa jumla na
rejareja.
Imeajiri
wafanyakazi 20 kwenye maduka yaliyopo Milenium Towers (Bidhaa Jumla), Mlimani
City Mall na Kibo Commercial Complex, Tegeta. Maduka haya yana bidhaa na
vipodozi aina mbali mbali zaidi ya 1000 yanayosambazwa nchini.
1 comment:
I all the time used to study article in news papers but
now as I am a user of internet so from now I am using net for posts,
thanks to web.
Post a Comment