Tangazo

April 12, 2012

MAZISHI YA KADA WA CCM, MAREHEMU GORDON MWAKITABU KATIKA PICHA

Vijana wa CCM wakibeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Ofisa Mwandamizi wa Makao Makuu ya CCM, Gordon Mwakitabu kuliingiza nyumbani kwa marehemu, eneo la Area C, mjini Dodoma leo, kwa ajili ya kuaga na mazishi yaliyofanyika baadaye kwenye makaburi ya Nkhungu nje kidogo ya mji. Aliyebeba msalaba ni mtoto wa kwanza wa marehemu Mwakitabu, Martin Mwakitabu.

Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mukama (katikati) akizungumza na Makatibu Wakuu wastaafu wa CCM, Philip Mangula (kushoto) na Yussuf Makamba, wakati wa shughuli za maziko ya aliyekuwa Ofisa Mwandamizi Makao Makuu ya CCM, Gordon Mwakitabu mjini Dodoma leo.

Mjane wa Gordon Mwakitabu, Janeth Mwakitabu akiangua kilio wakati wa kuaga mwili wa marehemu mumewe, leo nyumbani kwao, Area C, mjini Dodoma.

Waombolezaji wakiwa nyumbani kwa marehemu Mwakitabu wakati wa kuaga.

Makatibu wakuu wastaafu wa CCM, Yussuf Makamba na Philip Mangula wakiuaga mwili wa marehemu Mwakitabu.

Waombolezaji wakiwa katika huzuni na mshangao, wakati wa kuaga mwili wa marehemu Mwakitabu. Waliokaa mbele, Kutoka Kushoto ni Katibu wa NEC, Mambo ya Nje, Januari Makamba, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara), John Chiligati.

No comments: