Tangazo

April 16, 2012

Vodacom Tanzania yapunguza gharama za kutoa fedha katika huduma yake ya M-Pesa hadi asilimia 20

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza
Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania imepunguza gharama zake za  kutoa fedha kwa kupitia huduma yake ya m-pesa hadi asilimia 20 ambapo mteja anapotoa fedha kutoka kwa wakala yeyote wa M-Pesa.

Gharama hizi zimepunguzwa rasmi kuanzia tarehe 16 Aprili, Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Bw. Rene Meza alisema wateja wa Vodacom sasa wanao uwezo wa kutoa fedha kutoka kwa wakala yeyote nchini na watatozwa kwa hizi gharama mpya na nafuu zitakazosaidia zaidi shughuli za kiuchumi na kijamii za watu waliosajiliwa na huduma ya Vodacom M-PESA .

“Tunaelewa hali ya uchumi nchini na tunafahamu jinsi m-pesa ilivyokua huduma muhimu na bora katika maisha ya kila siku ya Watanzania, Hivyo tumeamua kuifanya iwe nafuu zaidi na rahisi kwa wateja wetu ”, alisema Mkurugenzi huyo katika taarifa iliyotolewa ya kutambulisha gharama mpya za kutoa fedha. ‘Hili ni lengo letu muhimu mwaka huu na zaidi” alisisitiza Bw. Meza.

Upunguzaji huu umekuja miezi michache baada ya Kampuni  kupunguza gharama za kutuma fedha na kuwa ndogo kwa kiasi cha kuanzia shilingi 50 kwa muamala na kuzindua promosheni ya siku 90 iitwayo ‘tuma na ushinde’ ambapo shilingi milioni 480 zitashindaniwa kwa kipindi chote cha promosheni.

Jukumu  letu ni kuhakikisha kwamba wateja wetu wana furaha na wanajiwezesha kupitia huduma  ya m-pesa. Tutaendelea kuboresha bidhaa na huduma zetu ambazo tunatoa kwenye m-pesa ili  kuhakikisha  umuhimu kwa maisha ya kila siku ya wateja alisisitiza Bw Meza.

Vodacom m-pesa inatoa huduma mbalimbali ikiwa ni pamoja na malipo ya bili kama vile LUKU, DAWASCO, DSTV na hata ada za mitihani ya NECTA. Vilevile inaweza kutumika kulipia  tiketi, safari za ndani  za ndege  za Precision Air na Coastal , ununuzi wa tiketi za basi, kulipa ada za shule, kuweka na kutoa fedha kupitia Benki ya CRDB, Western Union na huduma zingine nyingi.

Vodacom m-pesa ina  mtandao wa mawakala zaidi ya 20,000 Tanzania nzima, hakuna shaka kwamba Vodacom m-pesa ni huduma inayoongoza katika ufumbuzi na umaarufu na matumizi ya kuongezeka siku hadi siku na kufanya Vodacom Tanzania  iwe chaguo zaidi la ufumbuzi  wa  masuala ya fedha hapa nchini.

No comments: