Tangazo

April 12, 2012

WAJUMBE WA TUME YA MABADILIKO YA KATIBA KUAPISHWA NA RAIS KIKWETE KESHO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, atawaapisha Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Kesho tarehe 13 April, 2012, saa 3 asubuhi katika viwanja vya Ikulu.

Tume itaanza kazi zake rasmi tarehe 1, Mei, 2012 kama ilivyopangwa na kutangazwa awali.

Kwa kuzingatia umuhimu wa shughuli hii, Nawaomba wahariri mtutumie majina ya waandishi waandamizi ambao watafika ikulu mapema saa 2.00 asubuhi kwa ajili ya shughuli hii.

Tunaomba majina hayo ya wawakilishi wa vyombo vyenu yawasilishwe kwetu mara baada ya kupata taarifa hii na mwisho wakupokea majina itakuwa  saa 12.00 jioni ya leo.

Tunapenda kusisitiza kuwa waandishi watakaoruhusiwa kuhudhuria shughuli hii ni wale tu ambao tutapokea majina yao kutoka kwa wahariri wa vyombo husika.

Tunaomba ushirikiano wenu na karibuni.
 
Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi.
Ikulu-Dar-Es-Salaam
12 April, 2012

No comments: