Tangazo

May 22, 2012

Mchoro wa kumkejeli Zuma waharibiwa

Mchoro wa rais Jacob Zuma
Mchoro unaoonyesha uume wa rais wa Afrika Kusini Jaocb Zuma ukiwa nje, umeharibiwa.

Mchoro huo umezua utata nchini Afrika Kusini hasa baada ya kuwekwa katika jumba moja la maonyesho kwa umma.

Mtu mmoja amewagia rangi nyeusi mchoro huo na akaambia BBC kuwa unamvunjia heshima rais wa nchi hiyo.

Mwandishi wa BBC aliyekuwepo kwenye jumba hilo, anasema kuwa washukiwa wawili wamekamatwa.

Hapo awali, chama tawala kiliitaka mahakama kuu kulazimisha wanaosimamia maonyesho hayo, kuondoa mchoro huo.

ANC kilisema mchoro wenyewe ni kumvunjia hesgima rais na pia unakera. Hata hivyo wenye maonyesho wansema kuwa kazi yao inalindwa na katiba ambayo inaruhusu watu haki ya kujielezea.

No comments: