Tangazo

June 18, 2012

MWILI WA MAREHEMU WILLY EDWARD UKITOLEWA MOCHWARI MOROGORO TAYARI KUSAFIRISHWA KWENDA DAR

Kaka mkubwa wa marehemu aliyekuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward Ogunde, George Ongiri Ogunde (wa kwanza kulia) akishirikiana na ndugu, jamaa na waandishi wa habari, kubeba mwili wa mhariri huyo, aliyefariki dunia ghafla jana usiku eneo la Forest Hill, mjini Morogoro. Mwili huo ulikuwa unatolewa chumba cha kuhifadhia maiti Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Morogoro kwa ajili ya kusafirishwa kwenda jijini Dar es Salaam kwa maandalizi ya mazishi katika Kijiji cha Mugumu kilichopo wilaya ya Serengeti, mkoani, Mara.

Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (kulia) akisikiliza jambo kutoka kwa kaka mkubwa wa marehemu aliyekuwa mhariri mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward Ogunde, George Ongiri Ogunde muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kwenda jijini Dar es Salaam kwa maandalizi ya mazishi katika kijiji cha cha Mgumo kilichopo wilaya ya Serengeti mkoani Musoma. wa pili kutoka kulia ni Katibu Tawala wilaya ya Morogoro, Alfred Shao na kaka mkubwa upande wa baba, Isack Ugunde.PICHA KWA HISANI YA JUMA MTANDA BLOG

No comments: