******************
MSANII wa filamu nchini Visent Kigos 'Ray' amezindua filamu yake mpya inayojulikana kama 'SOBING SOUND'.
Filamu hiyo ameizindua kwa staili tofauti ambapo badala ya kuzindua ukumbini kama ilivyozoeleka na wengi, msanii huyo amezindua filamu hiyo katika kituo cha watoto yatima cha Maunga Centre kwa kutoa msaada wa vitu mbalimbali vyenye thamani ya sh. milioni 1.5/- kwa niaba ya Kempuni ya Steps Entatainment ya jijini Dar es salaam.
Akizungumza mara baada ya kuzindua filamu hiyo, Ray alisema ameamua kufanya hivyo kutokana na ukweli kwamba watu wengi wamekuwa wakifurahia maisha huku wengine wakiendelea kutahabika kitendo ambacho si kizuri.
" Ujio wa filamu hii ni kama azma yangu niliyoipanga tangu awali kuhakikisha filamu zangu zote zinafanya vizuri na ntakuwa kila filamu ntakayotoa nitahakikisha japo kidogo kwa namna yoyote nawakumbuka watoto yatima kwani nawajapenda", alisema.
Aidha alibainishwa kuwa kampuni ya Steps Entertaiment imekuwa msaada mkubwa kwa wasanii kutambulika na kuwashawishi wawe wanawakumbuka watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Naye Meneja Masoko wa Kampuni ya Steps, Ignatus Kambarage amesema swala la watoto yatima ni letu sote na wala halichagui kwa kuwa tuna wajibu na angalau kidogo tunachokipata kupitia filamu zetu tunarudisha kwa kutoa shukrani zetu.
Msanii wa Filamu Vicent Kigosi 'Ray' na Meneja Masoko wa Kampuni ya Steps, Ignatus Kambarage wakiwa katika picha ya pamoja watoto. |
No comments:
Post a Comment