Tangazo

June 19, 2012

Wajasiriamali 15 mkoani Mwanza wakabidhiwa Ruzuku kupitia kampeni ya TBL 'Safari Wezeshwa'

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Everist Ndikilo akimkabidhi Prudence Mubito mashine ya kusaga nafaka wakati wa kukabidhi zawadi kwa wajasilamali waliofuzu kupewa ruzuku za Safari Wezeshwa. Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya furahisha jijini Mwanza.Katikati ni Meneja wa Bia ya Safari Lager Oscar Shelukindo.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Everist Ndikilo akimkabidhi Aron Magembe Compresor mashine wakati wa kukabidhi zawadi kwa wajasilamali waliofuzu kupewa ruzuku za Safari Wezeshwa. Makabidhiano hayo yalifanyika mwishoni mwa wiki katika viwanja vya furahisha jijini Mwanza.Katikati ni Meneja wa Bia ya Safari Lager Oscar Shelukindo.
************************
Na Michael Machellah
MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi Evarist Ndikilo amewakabidhi rusuku wajasiliamali 15 katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza kufuatia program ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager ambayo inainua wajasiliamali kwa kuwapa vitendea kazi vya kupanua biashara zao.

Mhandisi Ndikilo aliwazkabidhi vitendeakazi mbalimbali kwa kila mtu kutokana na walivyoomba wenyewe ikiwa ni pamoja na mshine za kuranda mbao,friji,viti vya bar,meza,compresar za kupakia rangi,majiko ya kisasa,mashine ya kusaga nafaka,mashine ya kuoshea magari,mashine za msasa,vyerehani na vingine vingi.

Ndikilo aliishukuru kampuni ya Bia ya TBL kupitia bia yake ya Safari Lager kwa kufikiri jambo zuri kama hilo ambalo liko kwenye sera ya Taifa kwa kuinua kipato kwa wananchi hasa wanajishugulisha ambao wataisaidia majirani zao,jamii inayo wazunguka kwa kuwaajili na Serikali pia ambayo itafaidika kupitia kodi.

Alisema Ndikilo kazi kwenu sasa wajasiliamali mliowezeshwa kuwa mabalozi wazuri wa TBL haswa katika bia hiyo ya Safari Lager kuitangaza na kuinywa ili kurudidha walipotoa na kesho wawezeshwe na wenzenu.

Jumla ya watu 9638 waliomba kuwezeshwa lakini waliobahatika kwa Mkoa wa Mwanza ni 15 hivyo aliwataka waliokosa nafasi hiyo wasikate tama awamu nyingine waombe tena.

Nae Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo alisema mkataba wa ruzuku hizo ni wa miaka mitano hivyo watakuwa wakiwafuatilia wajasiliamali hao kujua maendeleo yao katika kipindi hicho chote wakiwasaidia wanapokwama na kuwaendeleza kuhakikisha wanainuka na kuinua jamii inyowazunguka.

Vifaa vilivyogawiwa kwa wajasiliamali wote vina thamaniya zaidi ya shilingi milioni 200.

No comments: